HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 22, 2013

MWIMBAJI NYOTA KUTOKA RWANDA, LILIAN KABAGANZA KUWASILI DESEMBA 23 KWA AJILI YA TAMASHA LA KRISMASI
Na Francis Dande
WAIMBAJI wa kimataifa wanaokuja kupamba Tamasha la Krismasi Desemba 25, wamezidi kuwasili ambapo Lilian Kabaganza kutoka Rwanda anawasili Desemba 23 kwa ajili ya tamasha hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo la kimatifa, Alex Msama, alisema Kabaganza anakuwa mwimbaji wa wa kuwasili akitanguliwa na Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mkubwa wa Kenya.

Kuhusu maandalizi, Msama alisema yamekamilika na kinachosubiriwa ni mashambulizi tu yatakayoanzia Uwanja wa Taifa Desemba 25 kabla ya kugeukia Motogoro, Tanga, Arusha na kuhitimishwa Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu ujio wa mwimbaji nyota wa nyimbo za injili kutoka Rwanda Lilian Kabaganza. 
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka Rwanda, Lilian Kabaganza ambaye anatarajiwa kuwasili Jumatatu Desemba 23 kwa ajili ya kushiriki katika Tamasha la Krismasi litakaloanza tarehe 25 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages