Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar (SMZ), Dk. Mohamed Shein
akimkabidhi tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Chiku Matesa kutokana na kutambua mchango wa shirika hilo wa kuchangia sh. milioni
100 wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar, uliokwenda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko huo. Hafla
hiyo ilifanyika mjini Zanzibar, mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kulia), Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (katikati), wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar, iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko huo.
Rais Dk, Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mashirika na Taasisi mbalimbali zilizochangia Mfuko wa Uwezeshaji Zanzibar.
No comments:
Post a Comment