MSIMU wa kwanza wa
Tamasha la Utamaduni Handeni, lililokuwa
likisubiriwa kwa hamu hatimaye lilifanyika Juzi, wilayani Handeni
Tanga ambapo kama ilivyokuwa ikitarajiwa, Shirika la Taifa la
mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilijitokeza na kubeba tamasha
hilo.
Meneja wa NSSF mkoani Tanga, Frank Maduga |
Shirika hilo, likiwa limejitokeza dakika za mwisho katoa udhamini wake
katika tamasha hilo kubwa na la kwanza kuwahi kufanyika katika Ardhi
ya wilaya ya Handeni linalojumuisha vijiji zaidi ya kumi, lilichangia
fedha taslimu shilingi milioni mbili, fedha ambazo kwa kiasi kikubwa
ukiacha mchango wa wahisani wengine zilichangia kufanikiwa kwa
Tamasha hilo.
Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali
waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la
utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema kukiwa na dalili zote za
tamasha kushindwa kufanyika kama ilivyotarajiwa, NSSF kupitia Ofisi ya
kanda ya Tanga ilijitolea kunusuru Jahazi.
Mratibu wa Tamasha la Utamaduni Handeni-Kambi Mbwana akitambulisha Wadhamini wa Tamasha hilo lililofanyika Juzi katika uwanja wa Azimio, wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. |
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akimkaribisha mmoja wa wahisani wa Tamasha |
JKT walikuwepo wakafanya yao jukwaani
ilikuwa ni noma saaaana
|
DC Muhingo Rweyemamu |
Shukurani kubwa
ziende kwa NSSF, kwa kweli hawa watu wanajali utu,
tunaomba watusamehe kwa mapungufu yetu lakini kwa kweli wanastahili
kuitwa mfuko wa Hifadhi,” alisema Kambi
Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake
lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao
pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa
Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha
kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo
wanayoyataka.
Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima
watu wa eneo Fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao
kwa sauti kama waratibu wa Tamasha hilo walivyofanya.
“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa
tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu,
Hongereni sana,” alisema Rweyemamu.
Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema
shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa
Tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika
kulitangaza Taifa.
Mamia ya Waandamanaji wakielekea katika Viwanja vya Azimio |
Taem Tamasha la Utamaduni Handeni....chezea |
No comments:
Post a Comment