HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2013

POLISI KILIMANJARO WANASA MTANDAO WA MAJAMBAZI
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha kwa wanahabari (hawako pichani) Bunduki aina ya Shortgun pamoja na Bastola aina ya Browning zilizokamatwa hivi karibuni zikihushwa katika matukio ya ujambazi. (Picha na Dixon Busagaga)

Na Dixon Busagaga,Moshi

POLISI mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kunasa mtandao wa watu
wanaodaiwa kujihusisha katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi na uporaji wa kutumia silaha za moto ya hivi karibuni baada ya kumkamata mtuhumiwa mwingine na kufanya idadi yao kufikia watano sasa.

Mbali na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo pia polisi wamefanikiwa kukamatabastola aina ya Browning yenye namba 0663 TZ CAR 75516 pamoja narisasi moja ya bastolailiyotambuliwa kuwa ni mali ya EvanceMasuki(54)mkazi wa Majengo mjini Moshi iliyoporwa na watuhumiwa hao October 12 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robrty Boaz alisema katikauchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa ,watu haowalikubalia kuonyesha silaha hizo pamoja na risasi tatu za Shortgunambayo inadaiwa kuhusika katika mauaji ya mfanyabiashara wa mbao mjinihapa Nickson Mushi.

“Katika hatua za uchunguzi tumebaini kuwepo uhusiano na ushiriki wasilaha aina ya shortgun katika mauaji ya mfanyabiashara Nickson Mushialiyeuawa huko maili sita Novemba tisa mwaka huu ambayo tunaifanyiauchunguzi wa kitaalamu.”alisema Boaz.

Boaz alisema pia wamefanikiwa kukamata komputa mpakato nyingine aina ya Toshiba ambayo iliibwa hivi karibuni toka kwenye duka liitwalo Pendeza mini super market mali ya William Mwacha mkazi wa mjini Moshi.

Kamanda Boaz aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja naEmanuel Makala(280 maarufu kama Rama,Seif Hussein(42)maarufu kama Mwamba ,Eben Mwaipopo(22)maarufu kama Hashimu,Nicolaus Urio(28) naEmmanuel Kiula(28) wote wakazi wa Moshi.

Boaz alitoa wito kwa wananchi waendelee kiimarisha vikundi vya ulinzikatika maeneo yao pamoja na kuwa wepesi wa kutoa taarifa za siri zaaharifu na uharifu kwa jeshi la polisi ili hatua ziweze kuchukuliwamapema kabla ya madahara kutokea.

Katika siku za karibuni katika mji wa Moshi na mikoa ya jirani
kumekuwa na matukio kadha wa kadha ya unyang’anyi na uharifu wakutumia silaha ambapo miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vikiporwa nipamoja na Laptop,Simu pamoja na fedha.

Juzi kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa, Koika Moita, aliwaambiawaandishi wa habari baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa watuhumiwa hao waujambazi ni pamoja na gari aina ya Toyota Mark II yenye namba T 564 AUW ambalo linaaminika kutumika katika kufanyia uharifu.

Vitu vingine ambavyo walikutwa navyo watuhumiwa hao mbali na bundukiaina ya Shrtgun pia walikutwa na laptop mbili aina ya Dell na Hpambazo  taarifa zinasema ziliporwa katika moja ya maduka yaliyopo jengo la Kibo tower mjini hapa.

Watuhumiwa hao pia walikutwa na vibao vitatu vya namba za gari (Platenumber) ambazo ni T916 ARK,vibao viwili na T885 AZW ambavyo vinadaiwakutumika mara wafanyapo tukio la uharifu kwa lengo la kujifichakunaswa na askari.

Pia watu hao walikutwa na funguo mbalimbali za magari,Simu nane zaaina mbalimbali ,vocha za mitandao mbalimbali ya simu ambazo thamaniyake haikuweza kufahamika mara moja pamoja na vifaa mbalimbavinavyoaminika kutumika katika  kuvunjia vikiwemo bisibisi,Nyundo,Prize  pamoja na Tindo 

No comments:

Post a Comment

Pages