Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka afrika Kusini, Solly Mahlangu (katikati) akicheza na mashabiki wake wakati wa tamasha la Krismasi lililofanyika kweny uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Solly akiwajibiki jukwaani.
Anitha Kijambula akiimba nyimbo ya Solly wakati wa tamasha hilo.
Tumaini Ntobo.
Kundi la The Voice likitumbuiza.
Mather Oliver akionesha umahiri wake.
Umati wa mashabiki uliojitokeza katika tamasha hilo.
Sarah Mvungi naye akuwa nyumba.
Edson Mwasabwite akiimba.
Tito Jackson akipokea zawadi ya CD kutoka wa Solly baada ya kucheza vizuri nyimbo za msanii huyo.
Solly Mahlangu akimtambulisha mke wake.
Tito Jackson akipokea zawadi ya CD kutoka wa Solly baada ya kucheza vizuri nyimbo za msanii huyo.
Solly Mahlangu akimtambulisha mke wake.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera na Uratibu Bunge), Williamu Lukuvi, amewataka waimbaji wa
nyimbo za Injili, kuiombea nchi iendelee kuwa katika amani, ili kila mmoja
aweze kufanyakazi zake bila hofu.
Lukuvi aliyasema hayo jijini
Dar es Salaam jana, wakati wa
Tamasha la Christmas 2013 lilliloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion.
Alisema pamoja na hayo, bado
serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kupigania amani ili kudumisha mshikamano
uliyojengeka kwa muda mrefu.
“Tunamuomba mungu andelee
kuiweka nchi katika amani ambayo itawafanya muendelee kuwa huru, kuitangaza
injili pia kuitangaza nje ya nchi.
“Namshukuru Msama kwa
kutukutanisha katika tamasha hili ambalo kwa mwaka huu ni la pili baada ya lile
la Pasaka, napongeza na kumtaka aendelee kuandaa matamasha hayo, ambako hata
serikali inatambua nyimbo hizo za Injili, ndio maana nilikubali kushiriki
tamasha hili.
Aidha, waimbaji wa tamasha
hilo walikuwa ni Bony Mwaitege, Rose Mhando, Edson Mwasabwite, Upendo Nkone,
Upendo Kilahilo, John Lisu, New Life Band na The Voice Acappella.
Wengine wa kutoaka nje ni
Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza na Ephraim Sekeleti ambako waimbaiji
Mwaitege, Mhando na Mahlangu walioneka kushangiliwa zaidi.
Mahlangu paboja na kutoa
burudani pia aliitumia siku ya jana kusherehekea siku ya kuzaliwa mke wake
ambapo aliamua kufanya hivyo kwa ajili kuheshimu mwaliko wa kuja Tanzania kwani
bila hivyo angeamuwa kubaki nyumbani kufanya sherehe hiyo ya mkewe.
Msama alimshukuru Waziri,
Lukuvi kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwani ni mara chache kwa baadhi ya
viongozi kukubali kuhudhuria sherehe kama hizo kwa madai ya kuwa na kazi
nyingine.
Aliongeza kuwa tamasha hilo
lingendelea jana mkoani Morogoro, kisha litahamia Tanga na kumalizia Arusha.
No comments:
Post a Comment