HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 26, 2013

WASANII KIBAO KUTUMBUIZA  MKOANI DODOMA 

 Mratibu wa Tamasha hilo John Banda akizungumza na Waandishi wa habari juu ya kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo, Kushoto ni Mmoja wa waimbaji kwenye tamasha hilo Beatrice Wiliam (BSS 2011) Maandalizi ya Tamasha la Chrismas ndani ya Dodoma tayari yamekamilika wasanii Kibao toka ndani na nje ya Tanzania wapo mkoani Dodoma na Asubuhi ya leo wameshiriki ibada ya pamoja katika kanisa la Mlima wa moto Sabasaba Dodoma.
 Josephine Sudai akionyesha uwezo wake wa kuimba ndani ya kanisa la mlima wa moto Dodoma kabla ya saa 7 mchana kuelekea uwanja wa Jamhuri kwenye tamasha la Chrismas
 Jubilee Lugobo toka jiji Dar es salaam nae yupo Dodoma kwa ajili ya tamasha hilo
  Lusekelo Mwandiga akiimba kwa mbwembwe ndani ya kanisa la mlima wa moto sabasaba Dodoma kabla ya kushiriki tamasha hilo
Mwanadada Rose Kimaryo ndani ya tamasha hilo na hapa ni mlima wa moto sabasaba
 Mwimbaji Beatrice Wiliamu akihojiwa katika moja ya Radio station IMPACT FM kuhusiana na Tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages