HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 23, 2013

TBL YAENDESHA SHINDANO LA UONJAJI BIA KWA WANAHABARI MWANZA
 Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza, Richmond Raymond, akimkabidhi zawadi  Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Wilhelm Mulinda (kulia) ,baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la kuonja bia, jijini Mwanza juzi.
 Mfanyakazi wa TBL Mwanza ambaye jina halikufahamika mra moja akimimina bia kabla ya shindano la kuonja bia kwa waandishi wa habari kuanza.
 Mshindi wa pili katika shindano la kuonja bia Miguel Suleman akipokea zawadi zake kutoka kwa Meneja wa TBL Mwanza, Raymond Richmond.
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuendesha zoezi la kuonja bia katika Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza juzi.
 Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima,Sitta Tumma akionja bia kwenye shindano la kuonja bia lililoandaliwa katika Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza juzi.
 Meneja Ubora wa TBL Jeremiah Kamambi, akitoa elimu kuhusu utengenezaji wa bia katika shindano la kuonja bia lililoendeshwa kwa waandishi wa habari na kampuni hiyo.
 Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Jijini Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TBL muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano la kuonja bia lililofanyika kiwandani hapo juzi.

No comments:

Post a Comment

Pages