Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndugulile amesema vijana
wakitumia michezo ipasvyo watajiepusha na janga la matumizi ya dawa za kulevya.
Dk Ndugulile alitoa kauli hiyo jana Mbagala jijini Dar esSalaam katika sherehe
ya kutimiza mwaka mmoja wa klabu ya mazoezi ya Mbagala Jogging.
Alisema kwa nafasi yake ya udaktari wa binadamu anafahamu umuhimu wa mazoezi
katika mwili wa binadamu hasa katika kupunguza vichocheo vinavyowaingiza vijana
katika tabia zisizostahili.
Mnaweza kujiepusha katika matumizi ya dawa za kulevya kwa kufanya mazoezi na
mkidanikiwa katika hili mtakuwa mmejiepusha kwa kiasi kikubwa na maradhi ya
ukimwi kwani kwa takwimuza manispaa yaTemeke kila wanawake watatu wanaojichoma
sindano za dawa ya kulevya wawili kati yao wameathirika kwa ugonjwa wa
ukimwi,huku katika kila wanaume watatu wenye kujidunga mmoja ameathirika
Kuhusu vijana kujiunga pamoja alisema wanaweza kutumia fursa hiyo kuanzisha
miradi itakayofadhikiwa na serikali
Katika maadhimisho hayo ya klabu ya mbagala Joging zaidi ya vilabu 40. kutoka
manispaa ya Temeke walishiriki kufanya mazoezi ya pamoja.
MBUNGE wa Kigamboni Dk Faustine Ndugulile akiwaongoza
wananchi mbali mbali wa wilaya ya Temeke waliojitokeza kushiriki sherehe
ya kutimiza mwaka mmoja kwa klabu ya
mazoezi ya Mbagala, vijana na wazee walishiriki katika joggin kabla ya hotuba
ya mbunge huyo.
Wakifanya mazoezi ya viungo.
Dk. Ndugulile akikata keki kuashiria kutimia kwa mwaka mmoja wa klabu ya Mbagala Jogging.
Mdau wa Mbagala Joggin kutoka gazeti la Tanzania Daima Abdallah Khamis akilishwa keki katika sherehe hizo.
Moshi Lusonzo kutoka gazeti la Nipashe linalomilikiwa na makampuni ya IPP naye alishiriki katika keki ya kutimiza mwaka mmoja kwa klabu ya Mbagala Jogging.
Dk Ndugulile akiwa na wanamichezo kutoka klabu ya Mbagala Jogging.
No comments:
Post a Comment