Mwanamuziki mkali wa kuandaa na kupangilia muziki mwenye uwezo wa kupiga ala zote za muziki, kama, Kinanda, Gitaa zote yaani Solo, Bass na Rhythim, na zaidi katika kukaanga 'Chips', kuzicharaza drams, Thabiti, Abdul, ameamua kuachana na kazi za kutumwa na badala yake ameamua kuunda kundi lake jipya la Taarab, linalokwenda kwa jina la Wakali wao.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Thabit, alisema kuwa kundi lake hadi sasa lina jumla ya wasanii 13, na linaendelea na mazoezi yake maeneo ya Kinondoni katika ukumbi wa Way Bar ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuandaa albam yao ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne.
Aidha alisema kuwa katika bendi hiyo iliyo chini ya Meneja wake, Godfrey Ngowi, hadi sasa imekwishaanza kufanya shoo katika baadhi ya maeneo huku ikiwa na waimbaji wengi wapya yaani Ma Under Ground, na wapiga vyombo aliowataja kwa majina kuwa ni Jumanne Ulaya, anayepiga solo, Shomari Zizu, anayepiga Gitaa la Bass, Omary Alli na Ndage Ndage, wanaopiga Kinanda.
Bendi hiyo inatarajia kutambulishwa rasmi mwezi Februari na kuzinduliwa ramsi mwezi wa nne katika Sikuku ya Pasaka, ambapo itazinduliwa rasmi bendi hiyo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Video zake, Albam na Vyombo vipya, ambapo kila shabiki atakayeingia getini atapatiwa Cd moja ya Audio yenye nyimbo za bendi hiyo.
Thabiti, alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Kalieni Viti Sio Umbea, Lipo Linalo Kusumbua, Mtu Mzima Hovyo na Subira Haina Kikomo.
ZAIDI BOFYA www.sufianimafoto.com
Thabit Abdul.
No comments:
Post a Comment