Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI wa kimataifa wa
nyimbo za injili ambao watahudumu katika Tamasha la Krismasi litakalozinduliwa
Desemba 25 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wameanza kuwasili
tayari kuwapa raha wapenzi, mashabiki na wadau.
Akithibitisha hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo la kimataifa, Alex
Msama (pichani), alisema waimbaji ambao wameshatua jijini Dar es Salaam ni Ephraim
Sekeleti kutoka Zambia na Solomoni Mkubwa kutoka Kenya.
Msama alisema kuwasili kwa
waimbaji hao ni faraja kubwa kwa kamati yake kwani ni mwanzo wa wengine kuanza
kuwasili kutoka Afrika Kusini na Rwanda.
Alisema mbali ya hao wa
kigeni, Malkia wa nyimbo za Injili Tanzania, Rose Muhando aliyekuwa nje ya nchi,
amerejea naye yupo jijini Dar es Salaam katika maandalizi ya mwisho kuelekea
tamasha hilo ambalo baada ya kuziduliwa uwanja wa Taifa, mashambulizi
yataendelea mikoani hadi Januari mosi.
Msama alisema baada ya tamasha
hilo kuzinduliwa Uwanja wa Taifa, mashambulizi yatahamia jijini Arusha, Morogoro
na Dodoma.
Kuhusu tiketi za tamasha
hilo, Msama alisema zitauzwa katika maduka ya Msama Promotions yaliyoko Mtaa wa
Mkwepu, Posta na Kariakoo, mtaa wa Masasi na Msimbazi karibu na Kanisa la Lutherani.
Maeneo mengine ni vituo vya
mafuta vya Puma Mwenge, Tangibovu na uwanja wa ndege, Best bite Namanga, ofisi
za Msama Promotions, Kinondoni Biafra, Wapo Radio na Praise Power redio.
Viingilio kwa VIP A ni sh 20,000,
VIP B ni sh 10,000, mzunguko ni sh 5,000 na watoto sh 2000 na mikoani ni sh 5,000 kwa wakubwa na watoto sh 2000.
Samahani ninashindwa kuelewa...Kama timu ya Simba wamewafunga Yanga inakuwaje wao (Simba) wapate TShs 1m na Yanga waliofungwa wapate TShs 98m? Naomba ufafanuzi, tafadhali.
ReplyDelete