Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
WATU wane wamejeruhiwa vibaya katika matukio mawili tofauti yaliyotokea kwa pamoja katika Mji mdogo wa Mbalizi nje kidogo mwa jiji la Mbeya likiwemo la nyumba 43 na vibanda vya biashara 35 na kanisa kuezuliwa na Kimbunga kilicho ambatana na mvua kali.
Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda wa matkio yote maiwili yaliyo ukumbu mji huo kwa wakati mmoja wanaeleza yote mawili kwa kupishana kwa muda mfupi kuanzia majira ya saa 7:34, mchana jana, hali iliyozua taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Akizungumza na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kutokea kwa matukio hayo, Diwani wa kata ya Utengule -Usongwe katika mji huo, Eliya Mkono, alisema licha ya matukio hayo kusababisha hasara kubwa hakuna mtu aliyekufa .
Alisema katika tukio la kwanza la Kimbunga kuezua nyumba za makazi ni watu wawili tu walijeruhiwa , akiwemo mwanamke mmoja aliyemtaja kwa jina la Salome Boniface ambaye ni mjamzito alijeruihiwa na kukimbizwa hospitali.
Alisema mwanamke huyo na majeruhi mwingine mwanaume ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kufahamika mara moja wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kukatwa na vipande vya bati na kwamba wamelazwa katika hospitali teule ya Ifisi.
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo, ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Godwini Kaunda, alisema maafa hayo yametokea katika vitongoji vitatu vya Mlimareli, Mtakuja, pamoja na kitongoji cha Chapakazi ambapo madhara makubwa ni uharibifu wa mali.
Alisema katika kitongiji cha Mlimareli, nyumba 10 zimeezuliwa kabisa mapaa yake, huku vibanda 16 mali ya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini vimeezuliwa kuzunguka eneo la kituo kikuu cha mabasi Mbalizi.
Alisema katika Kitongoji cha Mtakuja jumla ya nyumba 28 zimeharibiwa vibaya kwa kuezuliwa na kimbunga hicho, pamoja na vibanda vya biashara 17 katika soko la Mtakuja karibu na kambi ya jeshi la wananchi (JWTZ) Mbalizi.
Kwa upande wa kitongoji chas Chapakazi jumla ya tano zimezuliwa , likiwemo kanisa la EAGT la Mchungaji Mwasiposya ambalo nalo limeharibiwa vibaya.
Katika tukio la pili, Lori la mizigo aina ya volvoT 731 BLM lililokuwa likishuka mlima Iwambi katika mji huo liliyaparamia magari nane yaliyokuwa yameegeshwa kando ya barabara na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo kujeruhi watu wawili.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Stevini Satima , alisema Lori hilo
liliyaparamia magari hayo wakati likijaribu kulikwepa gari lkingine lililokuwa likikatiza barabara hiyo huku likiwa na shehena ya makreti ya bia.
Hata hivyo watu wawili t undo walijerhiwa ambao hata hivyo majina yao hayakufahamika mara moja na walikimbizwa katika hospitali teule ya Ifisi wilayani Mbeya Vijijini na walikuwa wakiendelea na matibabu.
Jambo Leo ilifanikiwa kuyaona magari matatu kati ya hayo nane yakiwa yameharibiwa vibaya, magari hayo ni T 367 ADR Toyota Hilux, Mark 11 lenye namba za usajiri T330 BRL, pamoja na Canter T 273 DRT ambayo yote yalikuwa yameharibiwa vibaya yakiwa eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment