Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela, amesemama, Ni mapema mno kusema Katiba Mpya itapatikana au Laa!
Mtetemela aliyasema hayo Jumatano April 2, mwaka huu alipozungumza na mwandishi asubuhi wakati akielekea kwenye vikao vya Kamati vya siku Tatu vilivyokuwa vinaendelea, ambapo alisema kwa sasa ni Mapema mno kusema Katiba mpya itapatikana au Laa!
Ndiyo kwanza tuko kwenye Vikao vya Kamati ambapo tunabanwa na Wakati hivyo kusema naweza kukaa tukazungumza kujibu maswali yako nitakuwa sikutendedi haki maana nitajibu haraka haraka, lakini nashukuru kwa kuwasiliana nam”.alisema Mtetemela.
Hata hivyo Askofu Mtetemela amewatoa Waiswasi wananchi akisema, kutokana na vikao vya kukaa pamoja vinavyoendelea Mungu anaweza kufanya Jambo lolote Jema kwa ajili ya Watanzania, lakini kinachotakiwa watanzania waendelee kuomba.
Mara baada ya Askofu huyo kufaulu kuwarejesha pamoja Wajumbe wa Bunge la Katiba waliogawanyika kimtazamo juu ya upigaji kura! Macho na Masikio ya Wananchi, yamekuwa yakielekea kwa Viongozi wa Dini hao, iwapo kuna ni Hekima nyingine itaoka kwao ili kuondoa Mpalaganyiko uliopo sasa kuhusu uhalali wa Sahihi za Mwalimu Nyerere naKarume.
Licha ya kuchangia katika Kanuni za Bunge na likaamua kutumia Kura zote ya siri na ya Wazi, Mtetemela pia alipata fursa kutoa nasaha kwa wajumbe kuwa wanapotosha umma kwa kelele zao bungeni; Hivyo hata alipoombwa na mwanishi kuelezea iwapo Katiba itapatikana au Laa! Hakujibu, isipokuwa kusema ni mapema mno.
Wiki iliyopita Askofu Mtetemela alisema Bunge la Katiba limeshatumia muda mwingi, lakini hakuna kitu ambacho kinaendelea zaidi ya kupiga kelele zisizo na maana, ambapo aliasa kwamba,
“Tatizo hatujakaa pamoja na kujua kilichotuleta hapa Dodoma. Watu hawaheshimiani, hawaheshimu kiti wala kutambua umuhimu wa uwepo wao hapa.. Naomba tubadilike sasa,” alisema Mtetemela.
No comments:
Post a Comment