HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2014

BONGO MOVIE YAWASAIDIA AKINA MAMA MWANA'NYAMALA

Na Elizabeth John
 
BONGO Movie Unit wameisaidia  wodi ya akinamama na watoto katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwa kutoa vitu vyenye thamani ya milioni 15 kama shukrani kwao kutokana na mafanikio waliyopata katika tasnia hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alisema, amua kufanvyo ili kurudishawalichouna kwa jamii inayowazunguka.

“Wasanii tunapata kipato kikubwa sana kutokana na sapoti ya jamii tunaamini kwa kufanya hivi mungu atatusaidia tunaweza tukavuna zaidi, pia ni kama shukrani kwa jamii kwa kutimiza miaka mitatu tau kuanzishwa Bongo Movie ianzishwe,” alisema.

Alisema katika msaada huo wametoa vitu mbalimbali kama, nguo za watoto, mabeseni, na vitu mbali ambavyo ni muhimu kwa mama na mtoto.

Baadhi ya wasanii ambao waliiwakilisha Bongo Movie ni pamoja na Steve Nyerere, Jacob Steven ‘JB’, Adam Kuambiana, Haji Adamu ‘Baba Haji’a wengine.


No comments:

Post a Comment

Pages