HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2014

KAJALA AWACHANA WANAOMFATILIA MWANAE

 Na Elizabeth John
MWANADADA anayetamba katika tasnia ya filamu nchini, Kajala Masanja ‘Kajala’, amewataka wanaomfatilia maisha yake na mwanae kukaa mbali na wao kwani hawajui ni shida gani amepata kumtunza mpaka kufikia hapo alipo.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Kajala aliandika kuwa, kuna watu ambao wanasema yeye anampotosha mwanae na kumfundisha tabia mbaya, hivyo amewataka kuacha kumsema vibaya mwanae waendelee kumsema yeye na sio mwanae.

“Hakuna kitu kinanikera kama kumsema vibaya mwanangu, hawajui ni jinsi gani nimemlea naomba waachane na maneno ya kijinga bora waniseme mimi sio mwanangu, Paulette, mimi nilikuwa naumia zamani lakini saivi nishazoea wamuache mwanangu kama namlea vibaya ni wangu wao hawausu,” aliandika staa huyo ambaye ameng’ara katika filamu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages