Meneja Msaidizi wa Bia ya Castle Lite, Geofrey Makau
(kulia), akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa Promosheni ya Castle Lite, Ratifu Komba tiketi ya kwenda nchini Afrika ya Kusini
kushuhudia Tamasha kubwa la TIMBALAND litakalofanyika nchini humo mwanzoni mwa
Mwezi Juni. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Castle Lite, Victoria Kimaro. (Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu
KINYWAJI cha Castle Lite
kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), jana imetaja majina ya
Watanzania 12 watakaoshuhudia ‘live’ onyesho la msanii maarufu duniani, Timothy
Zachery Mosley aliye maarufu kwa jina la Timbaland.
Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika
Johannesburg, Afrika Kusini hapo Juni, mwaka huu, huku watu hao 12 wakilipiwa
kila kitu ili kushuhudia mambo makali kutoka kwa msanii huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lite, Victoria Kimaro
alisema, wanajisikia faraja kupata watu hao waliotokana na promosheni
iliyoendeshwa nchi nzima.
Katika promosheni hiyo, wateja na
wapenzi wa Castle Lite walitakiwa kutuma namba zilizo chini ya kizibo cha bia
hiyo na hatimaye washindi kupatikana kupitia droo iliyofanyika.
“Kwetu kama Castle Lite tunawapongeza
s wateja hawa 12 ambao wamefanikiwa kuibuka kidedea katika promosheni hii
tuliyoizindua Januari na kumalizika Aprili 4.
“ Kama tulivyoahidi wakati
wa uzinduzi, washindi hawa wataondoka nchini Juni 6, mwaka huu kwenda Afrika
Kusini kushuhudia tamasha hilo.
“Washindi wetu watalipiwa gharama
zote za usafiri, malazi, chakula na usafiri wa ndani wakiwa huko na mambo yote
haya yatafanywa katika kiwango cha hali ya juu, yaani watachukuliwa kama watu
maalumu,” alisema.
Aliwataja washindi hao hao na sehemu
wanazotoka zikiwa kwenye mabano kuwa ni, Ratifu Gabriel Komba, William Yobu
Msangi, Emmanuel Mathayo Mushi na Amandi Mathayo Kimario ambao wote wanatoka
Dar es Salaam.
Wengine ni Bryson Evarist Temu,
Gabriel Pankrias Liyakurwa (Kilimanjaro), Kolman Julius Shayo (Mwanza), Fidelis
Festus Tesha (Dodoma) na Dickson Ladislaub Kanoni (Tabora).
Wapo pia Dorika Stephania Chirigati,
John Jackson Ringo na Frank John Zaburi ambao nao pia wanatoka Dar es Salaam.
Victoria, aliwataka washindi hao kuwa
mabalozi wazuri wa Castle Lite muda wote na aliwashukuru wote walioshiriki
katika promosheni hiyo.
Bia ya Castle Lite inazalishwa na
kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
No comments:
Post a Comment