MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Karama Masoud
‘Kalapina’ amesema kwasasa yeye ni msanii wa kimataifa ndio maana ameamua
kubadilisha staili yake ya uimbaji ili kutafuta soko zuri zaidi.
Msanii huyo kwasasa ametoa wimbo wake unaojulikana kwa jina
la ‘Hip Hop is Alive’ aliomshirikisha mkali wa muziki huo, Abubakar Katwila ‘Q
Chillah’ ambapo ametumia staili mpya tofauti na zile za awali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Kalapina alisema,
kwasasa amekuwa msanii wa kimataifa ndio maana anaamua kuukuza muziki wake kwa
kuwashirikisha wasanii wakubwa na kuzifanya kazi zake ziwe za kimataifa.
“Kalapina ni yuleyule sema wa sasa ni wa kimataifa zaidi,
nazidi kwenda kwenye viwango vya kimataifa zaidi,” alisema.
Msanii huyo ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri
katika tasnia ya muziki huo kutokana na ubora wa mashairi anayoyaandaa
kukubalika katika jamii inayomzunguka.
No comments:
Post a Comment