Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa hip hop nchini, Ibrahim
Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amevilalamikia baadhi ya vyombo vya habari kwa kukataa
kupiga wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la ‘KKK’ mpaka atakapofuta baadhi
ya mashairi ya wimbo huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Roma
alisema kwa kuwa anahitaji wimbo wake upigwe redio zote, amelazimika kufuta
baadhi ya vipande hivyo vya mashairi.
“Nashukuru Mungu wimbo wangu umepokewa
vizuri na unapigwa sehemu mbalimbali, ingawa kuna changamoto ambazo nimekutana
nazo lakini najua ndio maisha yanavyoenda hivyo ni kawaida tu,”.
“Mimi nyimbo zangu huwa zinaongea ukweli na
unaeyafanya hayo ukisikia lazima utapata hasira kutokana na hilo baadhi ya Ma
DJ wakawa wanagoma kuupiga ndio sababu ya kupunguza mashairi ya wimbo huo,”
alisema Roma kwa masikitiko.
Roma ni kati ya wasanii ambao wanafanya
vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na ubora wa mashairi ambayo
anayatunga na kukubalika katika jamii.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment