Kavumbagu alitua Yanga mwaka
2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika misimu miwili ya kuichezea klabu
hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote.
Kwa mujibu wa mtandao wa Azam
FC, wameingia mkataba wa mwaka mmoja na nyota huyo raia wa Burundi, wenye
kipengele cha kuongezewa mwaka mwingine, iwapo atafanya vizuri katika mwaka
wake wa kwanza.
“Tumepata mshambuliaji mzuri,
ambaye tayari ana uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa misimu miwili,
mchezaji huyu ni chaguo la Kocha wetu Joseph Omog, ambaye alivutiwa naye baada
ya kumuona akichezea klabu yake ya zamani, Yanga SC,” alisema Katibu Mkuu wa Azam
FC, Nassor Idrisa.
Kwa upande wake, Kavumbagu
alisema, yeye ni mchezaji, kazi yake ni mpira na amemaliza mkataba Yanga,
lakini viongozi hawamwambii kitu, hivyo amepata ofa nzuri Azam na kuamua kusaini.
No comments:
Post a Comment