HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 05, 2014

KINANA AINGILIA KATI MGOGORO WA SHAMBA LA EFATA NA WANANCHI SUMBAWANGA
 Mkazi wa Kijiji cha Mawenzusi, Kata ya Molo, Nuru Togwa akionesha jinsi masikio yake yalivyokatwa na anayedaiwa kuwa mwekezaji wa shamba lililokuwa la wananchi na kumilikishwa Shirika la Chakula la Taifa (NAFCO) na baadaye shamba hilo kuuziwa mwekezaji huyo Shirika la EFATA.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na mmoja wa wanakijiji cha Mawenzusi alipowasili katika kijiji hicho, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.Mwanakijiji huyo ameshika karatasi lenye maandishi yenye kilio cha kutaka wanakijiji hao kurejeshewa shamba hilo yenye ukubwa wa heka 10,000. Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili wananchi warejeshewe haraka shamba hilo.
 Kinana akiwa na wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mawenzusi
 Wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii cha chama hicho baada ya wanachama wapya zaidi ya 300 kukabidhiwa kadi za CCM baada ya kujiunga.
 Sehemu ya umati wa wananchi ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (katikati) alipokuwa akiwahutubia katika Kijiji cha Mawenzusi.
 Mjumbe wa NEC/CCM, Ally Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwataka wananchi kuudumisha muungano wa Serikali mbili badala ya tatu aliyodai kuwa ni mzigo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa ,Hypolitus Matete na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Hilary Aeshi katika mkutano huo wa hadhara.
 Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Kanondo kikitumbuiza katika mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya shamba la EFATA linaliotakiwa kurejeshwa kwa wananchi katika Kijiji cha Mawenzusi, Kata ya Molo, Sumbawanga Mjini. Picha na Kamanda wa Matukio Blog.

No comments:

Post a Comment

Pages