HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2014

MAFUNZO YA KUPUNGUZA MADHARA YA MAAFA NA KUTOA MSAADA WA DHARURA 
 Na Mwandishi Wetu

Wito huo umetolewa na Afisa Kilimo, Chakula na Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Valerian Vitalis Kidole katika semina ya waandishi wa habari inayoendelea katika ukumbi wa Kartasi uliopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kidole alisema kuwa ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia vyakula vile vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri vyakula vya msaada kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.

Hayo yamezungumzwa katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa Msaada wa Dharura yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio jamii yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa mada ya Usalama wa Chakula nchini.

 Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada wa chakula kwa wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika maeneo husika.

Aidha Kidole amesema kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali  ni nafaka ambayo hayawezi  kuboresha afya zao.

Katika halmashauri za mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula,  viongozi wa ngazi husika hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao mengi yanayohimili hali ya hewa husika na kwa wakati mwafaka ili kupunguza tatizo la upungufu wa chakula katika maeneo yao. Ni kwa namna hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa chakula cha msaada na badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages