HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2014

SEMINA YA UWEKEZAJI YA BENKI YA CRDB YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alipowasili katika hoteli ya Ledger kuhudhuria semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau na  wawekezaji katika sekta ya fedha.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Katibu wa Benki ya CRDB.
   Naibu Waziri waFedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
 Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau na  wawekezaji katika sekta ya fedha.
 Tunafuatilia mkutano......
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa mada wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha. 
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akifungua semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha. 
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Washiriki na wadau wa semina hiyo.
  Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akifuatilia kwa makini semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa mada wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akiteta jambo ma Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima.
 Naibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya uwezekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kufungua semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi wa wakurugenzi ya Benki ya CRDB. Martin Mmari akizungumza na waandishi wa habari.


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imezitaka benki nchini kupanua huduma za kifedha kwa wananchi ili kuweza kufanikisha ukuaji wa uchumi kwa maendeleo ya Taifa.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa taarifa za kifedha kwa wadau na wawekezaji kwenye sekta ya fedha benki ya CRDB,  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alisema, watanzania wanaonufaika na huduma za benki ni wachache lakini huduma za kifedha ni wengi hivyo kupanua wigo utaongeza upatikanaji wa fedha kwa urahisi.

Alisema sekta ya benki inamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo na ndo maana CRDB imeweza kuwaita wawekezaji wengi ili kuwekeza kwenye sekta muhimu ya fedha na yenye tija katika jamii .

“Jambo kubwa na la muhimu tunataka watanzania waweze kunufaika na huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa, wajibu wenu sasa CRDB kuendelea na utafiti ili kujua ni kwa namna gani mtaweza kuwafikia watu wengi zaidi katika huduma hizi za kibenki zenye lengo la kukuza uchumi wa nchi,” alisema.

Aidha alisema pamoja na uchumi wa Dunia kuteteleka lakini Tanzania aikuteteleka hiyo ni kutoka na kuwa na huduma bora na za uhakika zinazotolewa na benki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei, alisema  utoaji wa taarifa za kifedha pamoja na uchambuzi wa kina unasaidia kuona muelekeo wa benki jinsi ulivyo hivyo wameamua kukalibisha wawekezaji wengi katika soko la hisa ili kuweza kukuza uchumi.  

“Mwaka huu tumekaribisha wawekezaji wengi zaidi kwenye soko la hisa hiyo ni kwasababu mwaka jana tulifanya vizuri na kuingiza faida nyingi hata hivyo rasilimali za benki zimekuwa kwa asilimia 17 na bado zinaendelea kuongezeka zaidi,” alisema

Alisema uwongezekaji wa faida unatoka na kuwa na mazingira mazuri ya kiuchumi na wateja kukubali huduma za kibenki kwani uhamini zaidi huduma zao na kuzipenda.

No comments:

Post a Comment

Pages