Ayub Semtawa |
TIMU ya mpira wa miguu ST Gangwe ya Kicheba wilayani Muheza,Tanga, inatarajia
kufanya kumbukumbu ya kuwakumbuka wachezaji wake walioichezea timu hiyo kwa
mafanikio makubwa wakati wa uhai wao.
Kumbukumbu hiyo itafanyika kijijini hapo Aprili
11 mwaka huu, Siku ya Ijumaa Kuu kwa kuwashirikisha viongozi wakidini na vyama
mbalimbali vya siasa.
Akizungumza kwa njia simu na Tanzania Daima
mwishoni mwa wiki, Mratibu wa Kumbukumbu hiyo, Mustafa Mwinjuma (Wachuma),
alisema siku hiyo wameandaa michezo mbalimbali ikiwahusisha na wazee.
Aliwataja baadhi ya wachezaji watakaokumbukwa
siku hiyo kuwa ni Idrissa Semtawa ambaye ni baba mzazi wa mchezaji wa Coast
Union ya Tanga Ayub Semtawa, Omar Semhunge (Hondohondo), Hassan Bondo, Shah
Mussa, Mustafa Semtawa (Bob Wario) na
Stephen Kisingi.
Wengine ni Zuberi Mohamed (Mangasini), Mariamu
Hiza (Mama wa Gangwe), Godfrey Mwamlongo, Ayub Sekoba, Mwinchumu Mwinyiheri, Hatib
Hombo, Rawlance Raymond, Salehe Mhina, Salumu Azizi na wengingine.
Wachuma alisema siku hiyo viongozi wa wadini mbalimbali
watatumia nafasi zao kusoma visomo vya kuwaombea marehemu hao.
Alisema baada ya shuhuli hizo za ibada kutakuwa
na michezo ya mpira wa miguu, netboli, basketball, bao na ngumi zitakazo
simamiwa na bondia maarufu Abel Kisuse (Abel Boy).
Wachuma, alisema mechi itakayowavuta wengi ni
kati ya wapinzani wa jadi katika kijiji hicho yani ST Gangwe na Kicheba Stars
ambayo itapigwa saa 10:30 jioni kwenye uwanja wa Lusanga (Sululele).
No comments:
Post a Comment