Na
Elizabeth John
BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, Ally Mohamed ‘Z Anto’
amesema ukimya wake umesababishwa na kufiwa na mama yake mzazi aliyefariki
Julai, mwaka jana.
Z Anto ni kati ya
wasanii ambao walifanya vizuri miaka ya nyuma kutokana na ubora wa kazi zake
ambazo zilikuwa na mvuto kwa jamii inayomzunguka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Z Anto alisema,
aliamua kuwa kimya kwa lengo la kumkumbuka mama yake kwasababu alimpenda sana
na hakutarajia kama atampoteza kwa kipindi hicho.
“Nililazimika sana kukaa kimya kwasababu ya kumpoteza bi
mkubwa, mara nyingi nikienda katika shoo zangu nilikuwa namletea zawadi
alivyoondoka sikuona sababu ya kuendelea kufanya muziki wakati nina uchungu,”
alisema.
Msanii huyo kwasasa anatamba na kibao chake kinachojulikana
kwa jina la ‘Ukipendwa Ringa’ ambao umeanza kufanya vizuri kutokana na ubora wa
mashairi yaliyosimama ndani yake.
Z Anto alishawahi kutamba na kazi zake kama, Binti Kiziwi,
Kisiwa cha Malavidavi, Mpenzi Jini na nyinginezo nyingi.
No comments:
Post a Comment