Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) kitengo cha ushuru wa bidhaa na forodha Mkoa wa Mbeya kimeteketeza kwa kuzifinyanga na kisha kuloweka kwenye maji shehena ya Sigara aina ya SM mali ya Kmpuni ya TCC zenye dhamani ya zaidi ya sh mil 30 zilikuwa zinasafirishwa kwenda Zambia lakini zimerejeshwa nchini kwa njia ya magendo.
Akizugumza katika ofisi za kitengo hicho zilizo katika jengo za mamlaka hiyo jiji Mbeya ambapo zoezi la kuteketeza sigara limefanyika, Meneja katika Kitengo hicho, Joseph Ruge alisema kuwa sigara hizo zilikamatwa katika matukio mawaili tofauti wakati wafanyakazi wakiwa katika katika doria za kawaida baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi Ruge alisema kuwa tukio na kwanza lilitokea Janurai 23 mwaka huu likihusisha gari namba T 980 CBW lilikuwa likivuta tela namba T445 BHF mali ya kampuni ya NAM Enteprises ya jiji Dar-es-salaamu ambalo lilitokea nchini Zambia likielekea jiji Dar-es-salaam lilikuwa likendeshwa na dereva Benfred Kingi.
Meneja huyo aliongeza kuwa gari hilo lilikamatwa katika eneo la Iwambi jiji Mbeya likiwa na box 60 za sigara aina hiyo likiwa limetokea nchini Zambia ambapo inadaiwa kuwa gari hilo lilkuwa limapakia mizigo mingine vikiwemo vipodozi.
Aidha katika tukio la pili la linahusisha basi kamapuni ya TSK lenye namba za usajili T779 CSN linalo fanya safari zake Tunduma kwenda jiji Dar-es-salaam lilikamatwa Machi 23 mwaka huu katika kijiji cha Igawa Wilayani Mbarali likiwa na limepakia box tatu za Sigara hizo likotokea Tunduma.
Ruge alisema kuwa kwwa muda mrefu Mkoa wa Mbeya umeku moja ya vichochoro vya kuingizia
bidhaa hizo hapa nchini kinyume cha taratibu na Mamlaka husika zimekuwa zikiendesha msako wa kuzikamata zikiwa tayari sokoni jamboambalo pengine ndilo lililo ishitua mamlaka hiyo iliyo amua kuzidhibiti kuanzia zinakoingilia.
Meneja huyo alisema kuwa mbali na dhamani hiyo ya Sigala lakini wameteketeza malia ambayo imezaliswa
nchini kwa lengo la kuuzwa nje ya nchi lakini zikarudishwa kimagendo kinyume cha sheria hali iliyo liingizia Taifa hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 33 fedha ambazo zingelipwa kama ushuru ambapo box 63 ndanbi kukiwa na katoni 25 kwa kila box moja.
Kwa upande wake Meneja Kampmini ya Sigara hapa nchini (TCC) Mkoani Mbeya Wiliam Wiliam ambaye ni masahuhuda wa zoezi hilo alisema kuwa sigara hizo ni harali kwa matumizi ya binadamu lakini ilitengenezwa kwa soko la nje hivyo kitendo cha cha kuzirejesha ndani ya nchini kutaka kuuza kwa faida kwa kubwa kwani zinapunguzo la kodi na kinyume cha sheria.
Huku akionyesha baadhi ya alamu ambazo zinatambulisha kuwa sigara zilitengenezwa kwa ajili ya nje soka la Zambia ni stika za mamlaka ya matapo ya nchi hiyo ZRA huku zile zinapaswa kuuza katika soko la ndani zikiwa na stika zenye nembo ya mamlaka ya mapato nchi Tanzania TRA huku akibanishwa kmuwa kiwqanda kimekuwa kikiweka utatibu wa kuwqeka nembo kwa kila nchi ambako mzigo unapelekwa.
Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wafanyabishara hayo kuagiza mzigo huo unapelekwa nje lakini umerejeshwa ndani kwa lengo la kuuza kwa faida kubwa kwani bidhaa yoyote inayo zalishwa ndani inakuwa na punguzo la ushuru waforodha totauti na bidhaa zinazo uzwa katika soko la ndani.
Akizungumzia uamuzu wa kuteketeteza shehana hiyo kwa kutumia njia ya kuvunja na kisha kuziloweka kwenya maji tofauti na utaratibu ambao umezoeleka ambao umekuwa ukitumiwa na kwenye mizigo ambapo TRA huchoma, Williamu alisema kwa mjibu wa sheria za mazingira za kimataifa hairusiwi kwani zingeweza kuadhiri afya wa watu hivyo njia ya kuzifinyanga,kisha kuziloweka na baadaye kuzifukia katika shimo la taka ndiyo sahaihi.
Akihojiwa na waandishi wa habari sababu za kuchukua muda mrefu kuteketeza shehena hiyo tangu zilipo kamatwa Afisa mfawidhi wa forodha kituo cha Mbeya Magati Genda alisema kuwa ni kutokana kuchelewa kulipa faini kwa wamiliki wa magari ambapo kila mmoja alilipa dola za kimarekakani 5,000/ sawa na sh mil 8 kwa kila gari na mpaka sasa tayari zimeshalipwa na magari hayo yameshachukuliwa na wamiliki.
No comments:
Post a Comment