HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 21, 2014

Askofu Mshana: Uimbaji wa Kantate Usilipasue Kanisa!

Na Bryceson Mathias, Chamwino Dodoma

ASKOFU Msaidizi wa Dayosisi ya Dodoma wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Samwel Mshana, amewataka waimbaji kuelewa kuwa Uimbashaji wa Kantate ni wa kumsifu Mungu ili kukuza vipawa, na usifanywe kama Mashindano ya kupata Mshindi, jambo linaloweza kulipasua Kanisa.

Mshana aliyasema hayo katika Sherehe za uimbaji wa Mwimbieni Bwana Wimbo Mpya (Kantete-Domino) zinazofanyika kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu 2014 zilizofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Chamwino, Mei 18, 2014.

Akizungu na Waumini na Kwaya zote za KKKT Dayosisi ya Dodoma zilizoshiriki Uimbaji huo, Askofu Mshana alisema, Uimbaji wa Kantate ni wa kubaini Vipawa na kuviendeleza, hivyo kamwe usifanywe kama Mashindano na Matokeo yake ukalipasua Kanisa.

“Kuna mahali Kwaya zilishiriki Mashindano ya Uimbaji, mara baada ya Matokeo kutangazwa, hakuwa na maelewano, badala ya Mungu kutukuzwa Shetani alipata nafasi ya kusimika Uadui miongoni mwao kwa sababu tu ya kushindana na kutafuta Ushindi”.alionya Askofu Mshana.

Mshana alisisitiza kwamba, uimbaji unaotakiwa ni ule ambao Mwimbaji Stadi Daudi katika huduma yake ya uimbaji, alipoimba Viongozi wa Kanisa na Wafalme walipata Maono ya Kazi ya Mungu, Huzuni na Fadhaa zilitoweka.

Aidha Waumini na Waimbaji waliohudhuria Uimbaji huo, walimpongeza Askofu Mshana wakisema kwamba, Uimbaji wa Mashindano juu ya Neno la Mungu umepitwa na wakati kwa sababu unasababisha Magombano na Matengano miongoni mwa Waumini na Kwaya, wakashauri Kanisa liachane nayo.

Mmoja wa waumini wa Kanisa la Anglikani aliyehudhuria Uimbaji huo alisema, Kanisa lao limeuacha mtindo huo baada ya kusababisha utengano  siku za huko nyuma katika Kanisa lao, na hivi sasa wao wanafanya Matamasha ya Uimbaji ili kuhekimishana na kuinuana Vipaji.

No comments:

Post a Comment

Pages