HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 26, 2014

DAR WATESA MASHINDANO YA GOFU

Na Mwandishi Wetu

WACHEZAJI 14 kati ya 52 wa mchezo wa gofu wa Mkoa wa Dar es Salaam
ambao mwishoni mwa wiki walishiriki mashindano ya mchezo huo
yaliyojulikana kama 'Siku ya Gofu', waliibuka kidedea baada ya kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na BancABC.



Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na  BancABC,
yalifanyikia kwenye viwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ambao walizawadiwa vifaa mbalimbali vya kuchezea mchezo huo ni Peter Fiwa, Moses Namuhisa, Shaban Kibuna, Japhet Masai, Mohabe.



Nyirabu, Joseph Tango, Hitesh Valambia na Gabriel Abel, Olimpia
Flaten, F.Gwebe, A.Khamis, Rotsh, S.Denis  na g.Kasiga.
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Boniface Nyoni alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kutokana na kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini.


Nyoni alisema udhamini wao wa mashindano hayo kwa mwaka huu si mwanzo bali wataendelea kuyadhamini kila mwaka ili kuweza kuuendeleza mchezo huo nchini.

Alisema udhamini wao si kwenye mchezo wa gofu pekee bali ni katika michezo mbalimbali ikiwemo na soka.

Naye mmoja wa wachezaji walioshiriki mashindano hayo, George Nyakundi aliipongeza benki hiyo kwa kuamua kudhamini mashindano hayo na kuomba udhamini huo kutoishia mwaka huu.
"Kwa kweli sisi wachezaji wa mchezo wa gofu hatuna budi kupongeza

udhamini huu,hivyo na benki nyinge pamoaja na makampuni mengine yaige mfano huu,"alisema Nyakundi.

No comments:

Post a Comment

Pages