Kibao kionesha eneo la Hifadhi ya Mazingira ya Asili ya Chome Shengena Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira asilia Chome,William Nambiza akiwaonesha waandishi eneo lilillovamiwa na wachimbaji Madini na baadae walifanikiwa kuwaondoa, kwa siku walikuwa wanaingia zaidi ya 600,000 wakichanganyika na wa nchi jirani.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliofanya ziara ya kuona mazingira ya mto Chome ambalo ni chanzo cha maji yanayokwenda mto Saseni na kutoa maji kwa wakazi wa Same na kumwaga maji Bonde la umwagiliaji Ndungu,Ruvu na Pangani.
Meneja wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira asilia Chome,William Nambiza akiwaonesha waandishimiti waliopanda eneo la machimbo ya madini ya msitu wa Chome.
Meneja wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira asilia Chome,William Nambiza
akiwaonesha waandishi eneo lilillovamiwa na wachimbaji Madini na baadae
walifanikiwa kuwaondoa, kwa siku walikuwa wanaingia zaidi ya 600,000
wakichanganyika na wa nchi jirani.
Sehemu ya Msitu wa Chome ambayo ilichomwa Moto na wachimbaji Madini.
Sehemu ya Msitu wa Chome ulivyonawili.
Sehemu ya mpaka ya Msitu wa Chome na zilizokuwa na zisizokuwa za Msitu wa Hifadhi upande wa kulia.
Sehemu ya mpaka wa Msitu.
Sehemu ya Mto Saseni.
Sehemu ya Mto Saseni.
Sehemu ya mashamba ya wananchi wanaoishi karibu na mto Saseni.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
TAARIFA YA HIFADHI YA MAZINGIRA
ASILI CHOME
UTANGULIZI.
Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome (Shengena) ni msitu
wa Serikali Kuu unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika
Wizara ya Maliasili na Utalii. Msitu huu ulitangazwa kwa mara ya kwanza kuwa
Msitu wa Hifadhi mwaka 1951 kwa tangazo la Serikali Na. 125 la tarehe
25/05/1951. Ikafuatiwa na tamko la marekebisho kwa tangazo la Serikal Na 303 la
tarehe 20/06/1958.
Hifadhi hii ina ukubwa wa
eneo la Ha 14,283 na urefu wa mpaka wa Km
67. Hifadhi inazungukwa na vijiji 27 vilivyoko katika kata 11.
Katika kuhakikisha kuna usimamizi mzuri Msitu huu umegawanyika
katika safu tano za usimamizi ambazo ni Chome, Suji, Mamba miyamba, Bombo na
Mbaga.
MALENGO
Kutokana na mpago kazi wake hifadhi hii
ina malengo yafuatayo:
1 Kutunza mazingira asili, mfumo wa
ikologia katika uasilia wake.
2 Kuimarisha uhifadhi wa baianowai na
mtawanyiko wake.
3 Kuimarisha mfumo wa ekolojia.
4 Kulinda mmomonyoko wa udongo na
maporomoko ya ardhi na miamba.
5 Kuimarisha mafunzo na tafiti
mbalimbali.
6 Kushirikisha jamii na wadau wote
katika kulinda, kuhifadhi na kuendeleza uhifadhi.
7 Kuelimsha jamii
inyozunguka hifadhi njia mbadala ya kupunguza umaskini.
HALI YA AWALI YA HIFADHI
Hali ya Msitu huu ilikuwa na chnagamoto kubwa za uhifadhi ambazo
ni kama zifuatavyo;-
•
Uchimbaji wa
madini ndani ya hifadhi
•
Uchomaji
moto
•
Upasuaji wa
mbao
•
Uchungiji wa
mifugo
•
Ushiriki
mdogo wa wananchi katika kulinda hifadhi hii.
•
KUPADISHWA HADHI KUWA YA MAZINGIRA ASILIA
Kuna sababu nyingi za kimsingi na za kitaalam
zilizopelekea serikali kupandisha hadhi ya uhifadhi wa misitu huo kuwa hifadhi
ya mazingira asilia.
SABABU HIZO
NI KAMA IFUATAVYO:-
• Iligundulika
kuwa eneo hili lina bio-anuwai
nyingi za mimea na wanyama ambao ni
adimu, ndwele na wanaopatikana eneo hili tu.
• Eneo hili
linatunza maumbile ya asili na kuboresha
hali ya hewa na kuhifadhi gesi ukaa kuvuta mawingu yanayoleta mvua za mara kwa
mara.
•
Ni tanki la
maji kwa wakazi wanaozunguka hifadhi hii.
•
Ni kivutio
kwa watalii na hivyo utalii wa ekolojia unaendelezwa.
•
Ni sehemu
maalum kwa tafiti za ekolojia ya misitu ya tropiki.
HALI YA HIFADHI BAADA KUPANDISHWA
HADHI
Hatua hii ya kuupandisha Msitu na kuwa Hifadhi ya mazingira asili
kwa kiasi kikubwa imepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwa
zinaikabili hifadhi hii ambapo shughuli za uchimbaji wa madini
zimepungua,kutoka watu zaidi ya 40 kwa siku na kuwa na wastani wa mtu mmoja
hadi 4 kwa siku.matukio ya moto yamepungua pamoja na mifugo. Wananchi wameelewa
umuhimu wa utunzaji wa hifadhi.
Ili kuhakikisha kuwa uhifadhi unaendelea na hatimaye kufikia
malengo tajwa hapo juu hifadhi hii inafanya shuguli zifuatazo;
•
Kufanya
Doria shirikishi ndani na nje ya Hifadhi kwa kushirikiana na kamati za
maliasili za vijiji
•
Kuimarisha
mpaka wa hifadhi kwa kusafisha na kupanda miti.
•
Kurejesha
maeneo yaliyoharibiwakwa kufukia mashimo yaliyoachwa wazi na wachimbaji madini
haramu, kurudisha mikondo ya maji kwenye njia za asili na kupanda miti
•
Kuandaa na
kusafisha njia za kitalii
•
Kuwasaidia
wanavijiji kuanzisha bustani za miti ya asili kwaajili ya kupanda mashambani
•
Kuwawezesha
wanavijiji wanazunguka hifadhi kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiongezea
kipato mfano ufugaji nyuki,
•
Kuanzisha
Kamati za Maliasili za vijiji ili kuongeza ushiriki wa jamii zinazozunguka
hifadhi hii.
USHIRIKI WA TAASISI NA MASHIRIKA
MENGINE KATIKA UHIFADHI
Katika kuhakikisha kuwa hifadhi hii inatekeleza majukumu yake
kikamilifu hifadhi inashirikiana na taasisi na mashirika mbali mbali kama;-
•
Ofisi ya
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
•
Ofisi ya
mkuu wa wilaya Same
•
Ofisi ya
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Same.
•
Ofisi ya
mkuu wa kituo cha polisi Same
•
Mfuko wa
hifadhi ya milima ya Tao la mashariki (EAMCEF)
•
Shirika la
Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCG)
•
Serikali na
halmashauri za vijiji
•
Wananchi
wanaozunguka hifadhi
MAFANIKIO
Kwa kushrikiana na wadau wengine pamoja na serikali za vijiji
mafanikio yafuatayo yamepatikana kipindi
cha mwaka 2012 – 2014)
•
Kwa kufanya
doria shirikishi tumefanikiwa kuwaondoa wachimbaji wa madini ndani ya hifadhi
ambao walikuwa takribani 2000 na kufanikiwa kukamata zana mbalimbali
wanazotumia katika uchimbaji kama mashine za kusukumia maji (water pump) 20
Beleshi 30 Surulu10 n.k
•
Upasuaji
mbao umepungua ambapo kutokana na doria hizo misumeno 10 pamoja na wahalifu walikamatwa na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria pia mazao mbalimbali ya misitu yalikamatwa ikiwemo
milango 160 pamja na mbao vpande 100
•
Jumla ya
wahalifu 54 walikamatwa 16 kati yao wamehukumiwa vifungo vya kati ya mwaka
mmoja hadi miwili. 29 wamelipa faini 9 kesi zao bado zipo mahakamani.
•
Kuuongeza
ushiriki wa wananchi kwa kuanzisha Kamati za Maliasili za vijiji kwa kila
kijiji.ambazo jumla yao ni kamati 27.
•
Kuwaondoa
wavamizi wa hifadhi ambao walivamia kwa lengo la kulima au kuweka makazi ndani
ya hifadhi.
•
Kuimarisha
mpaka wa hifadhi kwa kupanda miti na kuweka mabango ili kuzuia uvamizi wa
hifadhi.
•
Kuwawezesha
wananchi kuanzisha bustani zao za miti ili kupanda katika mashamba yao.
•
Matukio ya
moto yaliyowahi kutokea yamepungua kutoka matukio 5 kwa mwaka hadi tukio moja
kwa siku.
•
Idadi ya
mifugo imezidi kupungua kutoka wastani wa ngombe 50 hadi wastani wa ngombe
watano wanaoingia ndani ya hifadhi.
CHANGAMOTO
•
Upungufu wa
rutuba katika mashamba ambao unasababisha jamii kutovuna mazao ya kutosha
kukidhi mahitaji yao.
•
Mtandao wa
wafanyabiashara wa mazao ya misitu hasa
mbao zinazokamatwa na miti comphour(mkulo) kwa kutengenezea milango , vitanda
n.k.
•
Kwa ujumla
wake ni matumizi dhidi ya uhifadhi.
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI KUJIONEA UTUNZAJI WA MISITU YA CHOME, SHENGENA-KILIMANJARO
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YANYA ZIARA NA WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI KUJIONEA UTUNZAJI WA MISITU YA CHOME, SHENGENA-KILIMANJARO
No comments:
Post a Comment