HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2014

HUSSEN MACHOZI AWATAYARISHA MASHABIKI WAKE

Na Elizabeth John
BAADA ya kuwa kimya muda mrefu, msanii wa bongo fleva, Hussein Rashid ‘Hussein Machozi’, amewataka mashabiki wa kazi zake kukaa mkao wa kula kwaajili ya kupokea kazi zake zinazofuata.
 
Katika wimbo huo unaojulikana kwa jina la ‘Utapenda’ amepanga kushirikiana vema na kundi la muziki huo lenye mafanikio makubwa Afrika kutoka nchini Kenya, Sauti Soul.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Machozi alisema wimbo huo kautengeneza katika Kampuni ya Ogopa Production ya jijini Nairobi, Kenya, chini ya mtayarishaji mahiri Adamu Juma, miezi kadhaa iliyopita.
 
Alisema wimbo huo unahusu zaidi mambo ya mapenzi, ambako kila mwimbaji aliyeimba anasifia mapenzi ya nchi yake, huku yeye akiwaeleza kundi hilo kwamba bongo kuna wanawake ambao wanajua kupenda kuliko nchi nyingine.
 
“Naomba wapenzi wa kazi zangu wanipokee vema katika soko na ujio wangu mpya, kwani mara nyingi katika nyimbo zangu huwa sipendi kushirikiana na msanii mwingine, naweza kusema huu ni wimbo wangu wa pili ambao nimeshirikisha mtu, mashabiki wategemee kazi nzuri,” alisema Machozi.

 
 
 

No comments:

Post a Comment

Pages