Na Elizabeth John
WAKATI kampeni maarufu ya ‘baki njia kuu, mchepuko sio dili’ ikiendelea nchini kuwahimiza wanandoa kuwa waaminifu kwa wenzi wao, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Moses Bushamaga ‘Mez B’ ameanzisha kampeni yake ya kusisitiza zaidi.
Kwa mujibu wa msanii huyo, wazo la kampeni hiyo lilikuja baada ya kuachia wimbo wake uitwao ‘Shemeji’ unaozungumzia jinsi shemeji yake alivyoisaliti ndoa yake.
“Nimeona hili ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu sasa hivi, watu wengi sana wanasaliti ndoa zao ba mahusiano yao, kwahiyo kwa kutumia nyimbo yangu nimeona nifanye kama kampeni ya kuhamasisha watu kutulia kwenye mahusiano yao,” alisema.
Alisema katika kuhakikisha kufanikisha hilo, atazunguka katika mikoa mitano nchini ikiwemo, Mtwara, Mbeya, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam na anatarajia kusindikizwa na wasanii wengine akiwemo mkali wa muziki huo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’.
Mkali huyo ambaye alikuwa ni mmoja wa wasanii waliokuwepo kwenye kundi la Chamber Squad lililokuwa likiongozwa na Marehemu Albart Mangweha, alishawahi kutamba na kazi zake kama ‘Kidela’, ‘Muziki Bongo’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
No comments:
Post a Comment