Na Mwandishi Wetu, Arusha
MBUNGE wa
Simanjiro ,Christopher Ole Sendeka ameitaka Wizara ya Nishati na Madini
kupitia waziri wake, Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa kina juu ya
kuondolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite waliopo mpakani kwa
madai kuwa wanachimba madini eneo la Tanzanite one.
Aidha baadhi ya wachimbaji hao walioko mpakani waliitwa na Kamishna Msaidizi Kanda ya Kaskazini, na kuwaagiza kuondoa miundombinu yao kwani wanachimba madini kwenye eneo la Tanzanite one na kutishiwa kufutiwa leseni wasipofanya hivyo.
Hata hivyo alipinga vikali amri iliyotolewa na wizara hiyo ya kusitisha uchimbaji wa madini ndani ya kitalu C inayopakana na tanzanite one,ambapo aliahidi kushughulikia maswala hayo bungeni na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi kulingana na sheria zilizopo.
Aidha kutokana na malamiko hayo, ililamzimu Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka kufanya mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo tawi la Mirerani pamoja na wadau wa madini ambapo alilaani vikali kitendo hicho kilichofanywa na wizara ya nishati na madini huku wakikiuka sheria na kanuni zilizopo.
Aidha aliitaka wizara hiyo kupitia kwa waziri wake Muhongo kutoa ufafanuzi wa kina na sheria waliyoitumia kuwataka wafanyabiashara hao kuondoka katika eneo hilo kwani huo ni uonevu mkubwa ambayo haipaswi kamwe kuvumiliwa .
Sendeka pia alishangazwa na hatua ya wafanyabiashara hao kutaka kufutiwa leseni kitendo ambacho ni uonevu mkubwa ndani ya nchi hii wakati sekta hiyo ya madini imeajiri idadi kubwa ya vijana ambao wamekuwa wakijishughulisha na biashara hiyo, na kusema kuwa kama leseni zitafutwa kwa wachimbaji na kwa tanzanite one pia zifutwe .
Aidha Sendeka aliitaka wizara kuacha mara moja utaratibu wa kusitisha leseni za wachimbaji wadogo kwani kufanya hivyo ni uonevu mkubwa ambao kamwe hautaweza kuvumiliwa na wadau mbalimbali wa madini .
Naye Katibu wa Marema Tawi la Mirerani ,Abubakari Madiwa alisema kuwa,malalamiko hayo wameshayatoa zaidi ya mara tatu kwa mbunge huyo na viongozi mbalimbali wa madini bila kupatiwa ufumbuzi wowote ambapo walimwomba mbunge huyo kwa mara nyingine tena kushughulikia malalamiko hayo ambayo yameleta athari kubwa kwa wachimbaji wadogo wa madini .
Hata hivyo waliomba kuondolewa kwa sheria ya wima na sheria hiyo kufutwa kabisa kwa manufaa ya wachimbaji wadogo wa Tanzanite,na hivyo kumwomba mbunge huyo kutatua tatizo la mpaka baina ya kitalu B na C ambao haujatatuliwa hadi sasa.
Pia waliomba kusitishwa mara moja kwa utartibu wa kufuta leseni kwa wachimbaji wadogo wa kitalu B na D kwani hii ni mbinu chafu inayofanywa na baadhi ya maofisa wa wizara ya nishati na madini wakishirikiana na kampuni ya tanzanite one ambayo ina utata wa umiliki wa leseni hiyo ya kitalu C.

No comments:
Post a Comment