Na Elizabeth John
MWILI wa aliyekuwa muigizaji na mtayarishaji wa filamu za
Bongo, Adam Kuambiana unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Leaders,
kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam jana,
msanii Haji Adam ‘Baba Haji’ alisema, marehemu ataanza kuagwa saa 3 asubuhi
katika viwanja hivyo kabla ya kupelekwa kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Alisema msiba wa marehemu unafanyika nyumbani kwake Bunju B
njia panda ya Magwepande.
Kuambiana ambaye nyota yake katika tasnia hiyo ndio ilikuwa
inaanza kung'ara kutokana na kuifanya kazi yake kwa uweledi wa hali ya juu,
imezimika gafla wakati bado mchango wake ukihitajika.
Msanii huyo ambaye
alikuwa anatatizo la vidonda vya tumbo, alifariki juzi katika hospitali ya Mama
Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam alipopelekwa baada ya kuzidiwa wakati
akiwa ‘location’ katika hotel ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy.
Kuambiana alianza
kusikia maumivu ya tumbo wakati yupo location wanapiga baadhi ya picha ya
filamu yake mpya ambayo aliwashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo msanii wa
Bongo Fleva, Q Chillah.
Baadhi ya filamu
ambazo alicheza na kuongoza Kuambiana ni pamoja na Danija,
Faith More Fire, Bad Luck, Scola,The Boss, Mr.Nobody, Radhi ya Mke, Lost
Sons, Chaguo Langu, My Fiance, Jesica, Life of Sandra,
Basilisa, My Flower, Regina, Born Again, Its Too Late, Fake Pastors, ‘Mr
Kadamanja’ na nyingine.
No comments:
Post a Comment