HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 26, 2014

NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA-TANGA
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Tanga, Frank Maduga (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda wakati alipotembelea banda la shirika hilo katika maonesho ya pili ya kibiashara yanayofanyika viwanja vya Tangamano jijini Tanga na kushiriki mataifa mbalimbali. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Ofisa Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Tanga, Athumani Juma (kulia) akiwasikiliza baadhi ya watu waliotembelea kwenye banda lao wakati wa maonesho ya pili ya kimataifa ya Biashara yaliyofunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara. Dk. Abdallah Kigoda.
 Ofisa Mwandamizi wa NSSF Makao MakuuTheopista Muheta (kulia),  akimsikiliza mmoja wa watu waliotembelea banda la NSSF wakati wa maonesho ya pili ya kimataifa ya kibiashara yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano Tanga. Wa pili kushoto ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Frank Maguda na Ofisa Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Tanga, Athumani Juma.
 Muuguzi, Elionora Mmasi akiwapima wanachama wa NSFF waliotembelea banda lao wakati wa maonesho ya pili ya kibiashara yanayofanyika mkoani Tanga.
Baadhi ya watu waliofika katika banda la NSSF wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Shirika hilo kuhusu Fao la Matibabu wakati wa maonesho ya pili wa kibiashara yanayofanyika mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment

Pages