HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2014

TIMU  YA KUOGELEA YAAHIDI MEDALI MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya taifa ya kuogelea itakayoweka kambi nchini New Zealand Juni 6 hadi Julai 17 mwaka huu imeonyesha matumaini ya kupata medali katika michuano ya Jumuiya ya Madola.

Akizungumza na Habari Mseto Blog, Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Noel Kiunsi amesema kuwa waogeleaji Mariam Foum, Ammaar Ghadiyali na Mangadalena Mushi wanaosoma  Australia, Canada na Misri wanaendelea na mazoezi makali ambayo yamewaweka katika kiwango kizuri cha kuvuna medali katika michuano hiyo.

Kiunsi alisema mbali na waogeleaji hao watatu pia nahodha wa timu hiyo, Hilal Hilal anasaka sekunde moja tu kujihakikishia kupata medali ya dhahabu katika mbio ya mita 50 freestyle.

“Hilal ambaye mwezi uliopita alipata medali ya dhahabu katika michuano ya CANA Kanda ya 3&4 kwa kutumia dakika 23 sasa anahitaji kushusha muda huo kwa sekunde moja ili kujihakikishia medali nyingine ya dhahabu katika michuano ya Madola,” alisema.

Wakati huo huo Kiunsi alisema waogeleaji Mariam, Ammaar na Mangadalena wanaendelea na mazoezi makali ya kupunguza muda wao walioweka rekodi katika mashindano ya kimataifa wakati wakisubili kumalizia mitihani ili waungane na Hilal aliyepo nchi akiwasubili waweze kwenda nchini New Zealand kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na michuano ya Madola.

No comments:

Post a Comment

Pages