Na Clezencia Tryphone
KAMPUNI ya Yuneda Intertainment inayojihusisha na shughuri
mbalimbali za Kijamii na Burudani imeingia makubaliano na Nchi zaidi ya 10
ikiwemo na Ufaransa ili kusambaza Filamu ikiwa na lengo la kubolesha kazi za
wasanii hapa kitaifa na Kimataifa Pia.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka nchini Ufaransa jana,
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Ngeze Mushi alisema, kwake ni faraja kupata, lakini
pia ni moja ya njia ya kufikia malengo waliyoyapanga kama kampuni ndani ya
mwaka huu kupitia kwa wasanii wanaofanya nao kazi.
Ngeze alisema, katika makubaliano yao na nchi hiyo,
wamekubaliana, filamu italipwa kulingana na ubora, urefu wa filamu, wachezaji
na mambo mengine mbalimbali huku Filamu moja inatarajia kuuzwa si chini ya dola
12,000.
“Kwa sasa tumekubaliana kuanza na filamu mbili ya ‘six
times two’ ambayo kwa Tanzania tutaitoa mwezi huu na ‘why Linah’ ambayo
Tanzania imeishatoka,”alisema Ngeze na kuongeza kuwa, wanaimani kwa sasa
wasanii watanufaika kupitia makubaliano hayo ya Yuneda na nchini hizo.
Ngeze alisema, kwa sasa Yuneda wanaanda CV za wasanii ili
wawe wanashiriki kwenye filamu nyingine nchini Ufaransa na kwingine, kwani
wanaimani kupitia hiyo, itakuwa mwanga kwa wasanii na kuwasaidia kukuza filamu
Tanzania na wasanii pia.
“kwa ufupi hii itakuwa neema kwa wasanii, nilikuja huku
tarehe 27, mwezi wa nne natarajia kurudi kuanzia tarehe 10 mwezi huu, kwa hatua
hii mimi naona ni moja ya hatua nzuri kwa Watanzania na wasanii wetu kwa
ujumla,”alisema Ngeze.
Alisema, kwa upande wa filamu kwa sasa wamesitisha kupokea
filamu kwa sababu watengenezaji hawana urafiki na wasambazaji, story za filamu
zanakuwa niza kuunga, ubora hautakuwa ule unaotakiwa kimataifa hivyo yuneda
entertainment watakuwa wanatengeneza wenyewe na kusambaza.
“Mwezi wa sita nitakuwa Afrika ya kusini na Canada kukutana
na wadau wa filamu na dhani na hii itakuwa fursa kwa wasanii na Yuneda
entertainment pia,”alisema na kuongeza kuwa nimefanikiwa kupata wadau wa
kitengo cha Yuneda entertainment pia nimepata wafaransa tutakao shirikiana
kwenye Yuneda microfanance na akramu real estate hawa watafika mwezi Agasti
kujadiri na kuangalia tuanzie wapi,
Naimani kampuni za kizalendo kwa nchi yetu kama ilivyo
yuneda inatakiwa kupata wadau kama hawa ilikuweza kukua kwa haraka.
No comments:
Post a Comment