MWILI wa aliyekuwa muasisi wa filamu za kibongo nchini, raia
wa Kenya George Otieno ‘George Tyson’ unatarajiwa kuagwa keshokutwa katika viwanja vya
Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alisema mwili wa
marehemu uliletwa Dar es Salaam Jumamosi na kuhifadhiwa katika hospitali ya
Kairuki, Kijitonyama.
Alisema shughuli za msiba zinaendelea nyumbani kwa marehemu,
Makongo na amewataka wasanii mbalimbali kujitoa katika shughuli hizo kwa
kipindi hiki kigumu.
“Tunatakiwa kushirikiana kwa kipindi hiki kigumu kila mmoja
anajua kama bongo movie tumepatwa na misiba ya ndugu zetu ambayo imeacha pengo
kubwa, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho kutwa (Jumatano)
kupelekwa kwao Kenya kwaajili ya mazishi,” alisema.
Tyson alikuwa mtayarishaji wa vipindi maarufu kama The One
Show na Mboni Talk Show alifariki dunia ijumaa usiku kwa ajali ya gari
iliyotokea eneo la Kibaigwa Wilayani Kongwa, Dodoma akirejea jijini Dar es
Salaam.
Msanii huyo ambaye alikuwa ni muongozaji na mtayarishaji wa
filamu hizo, alizaliwa mwaka 1973 nchini Kenya na aliwahi kuwa mume wa Yvony
Cherry ‘Monalisa’ na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike.
No comments:
Post a Comment