INASEMEKANA hela alizorusha msanii wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ katika shoo ya kuhamasisha usafi katika
Wilaya ya Temeke, ndio chanzo cha vurugu zilizotokea katika uwanja wa Mwembe
Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam.
Katika shoo hiyo iliyoanza saa 8 mchana katika viwanja hivyo, na
kutarajiwa kumaliza saa 12 jioni ilikatishwa kutokana na vurugu, ilikuwa
kwaajilili ya kuhamasisha usafi na kutambulisha video Mkude Simba huku
akisindikizwa na wasanii kibao ambao wanatamba katika tasnia hiyo.
Akizungumza mmoja wa wasanii ambao walikuwepo
katika tukio hilo, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema, chanzo
cha vurugu ni Dimpoz kurusha hela kwa mashabiki ambapo kila mmoja alitaka
kuzipata fedha hizo.
“Watu walijaa sana, nay eye aliporusha hela kila mmoja alitaka
kuzifikia hizo hela, Dimpoz aliposhuka alipanda Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ na
watu wakaanza kurusha chupa jukwaani na wakimtaka aondoke, polisi wakaingilia
kati na hapo vurugu ndipo zilipoanza,”.
Kwa upande wake Dully, alisema anasikitika sana kwa kuona watu
wanamuona yeye ndiye aliyeanzisha fujo katika shoo hiyo kitu ambacho sio kweli.
“Polisi na mabaunsa ndio walianzisha fujo, kwasababu walikuwa
wanawazuia watazamaji kusogea mbele kwa kuwapiga hivyo fujo ndio zilipoanza
watu wakaanza kurusha mawe, chupa na viatu polisi wakaamua kupiga mabomu ya
machozi watu wakaanza kusambaa na wengine kuumizana,” alisema Dully.
Naye Mussa Kitale ‘Kitale’ alisema, anawashukuru mashabiki
wake kwa kufika kwa wingi katika onesho hilo ambapo anasema aliamua kuonesha
tangazo moja tu kutokana na kuhofia vurugu baada ya kuona watu wamejaa sana.
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Englibert
Kiondo, na kutakiwa kuzungumzia hilo, simu yake ilipokelewa na sekretari wake
na kudai kamanda yupo kwenye kikao.
Shoo hiyo iliandaliwa na E Redio ikiwa ni kwaajili ya
kutambulisha redio hiyo pamoja na video za Mkude Simba ambazo zinarushwa katika
redio hiyo na Times Fm.
Wasanii ambao walikuwa wameshapanda jukwaani ni pamoja na Q
Chillah, Inspector Haroun, Shilole, Kitale, Ommy Dimpoz na Juma Nature.
No comments:
Post a Comment