HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2014

STARS YAWASILI AFRIKA KUSINI

Kikosi cha Stars
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
 
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya jioni kuanza safari ya Maputo.
 
Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
 
Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).

No comments:

Post a Comment

Pages