HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 23, 2014

Wachuuzi wa Ufuta Mbeya wakiri kuchanganya na Mchango

Na Keneth Ngelesi, Mbeya
WAKULIMA wa zao la Ufuta katika Wilaya za Mbozi na Chunya Mkoani Mbeya wameitaka Serikali kutoa bei elekezi ya zao hilo badala ya kuachia kazi  hiyo  makampuni makubwa ambayo hata hivyo hayatoi bei inayolingana na thamani ya mazao wanayo zalisha.

Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na wakulima hao wakati wakifanya mahojiano na Tanzania Daima  hivi karibuni kwa nyakati tofauti katika Mji wa Mbalizi, walisema kuwa kuna haja ya serikali kuanzisha utaratibu kutoa bei elekezi kama ilivyo kwa mazao mengine ya biashara ili kuepusha  unyonyaji unaofanywa na wachuuzi pamoja na  wafanyabishara wakubwa na Makampuni yanayo jihusisha na ununuzi wa zao hilo.

Lydia Mwali ni miongoni mwa wakulima wa zao la ufuta kutoka Wilaya ya Mbeya Vijijini ambaye alisema kuwa wachuuzi na wafanyabiashara kutoka Makampuni Makubwa wamekuwa wakinunua zao hilo kwa bei chini jambo amabalo haliwezi kumsadia mkulima aweze kupiga hatua ya kimaendeleo.

‘Sisi wakulima tuna nyanyasika sana tunauza Ufuta kwa bei ya chini mno na hata fedha tunazo pata haziwezi kutusaidia kitu kwani ni kidogo mno, hivyo kama kweli Serikali ina dhamira ya dhati na wakilima wa nchi hii ni vema ikawa na utaratibu wa kuwa na bei elekezi ili kutunusuru wakulima” alisema Mwali.

Alisema uuzaaji wa Ufuta kwa bei ya kutupwa inachangia kwa kiasi kikubwa wakulima kusahindwa kumudu gharama za kununua vitendea kazi kwa ajili ya uzalisha ndiyo maana wamekuwa wakitumia vyandarua vya kulalia vilitolewa kwa msaada kwa nchi ya Marekani kutumiwa kama chekecheo wakati wa kuvuna zao hilo.

Aliongeza kuwa kutokana na watu kutumia vyandarua hivyo kupepea ufuta hali hiyo imepekea zao hilo kushuka kiwango kila mwaka  huku likipoteza radha yake kutokana kuwa na taka nyingi huku ukiwa umechanganywa na mchanga ulioambatana na vumbi.

‘Walanguzi na wachuuzi ufuta wananunua kwa bei ya kutupwa ndiyo maana wakulima wanashindwa kumudu gharama za  vitendea kazi,kama nyungo kwa ajili ya kupepea,yahani huezi amini wakulima wengi tunatumia vyandarua vilitolewa na Bush kwa ajili kujikinga na Mbu wanaoeneza Malaria lakini sisi tunatumia kupepetea ufuta jambo ni hatari kwa afya zetu hata ubora wa zao lenyewe’ alisema Mwakalonge.

Kwa upande wake mmoja wa wachuuza ambao hununua Ufuta kutoka kwa wakulima na kuuza kwa  wafanya biashara wakubwa Alimu Mwakalonge akikiri kufanya ujanja huo wa kuchanganya mchanga,uwere  na ufuta na kwamba sababu za kufanyi hiyo ni kutokana na mizani wanayo tumia ni ya wafabiashara na imefanyiwa uchakachuaji.

Akifafanua zaidi alisema kuwa awali walikuwa wakitoka shamba na mazigo na gunia likiwa na ujazo wa kilo 140 lakini wanapo fika kupima kwenye mizani ya wafanyabisha hao wakubwa kilo 10 hupungu kwa kila gunia na mara baada ya kufanya uchunguzi walibaini mizani ya siyo sahihi.

Aliongeza ili kuondoa mvutano wao wamekuwa wakiongeza chepe tatu za mchanga ambazo ni sawa na kilo 10 ili kuidia upungufu huo na mara wanapofika  kupima kwa  kutumia mizani ya wafanyabiashara hao imekuwa haiwi pungufu.  

‘Yahani hii ni kama jino kwa jino hawa wenzetu wamenyonga mizani yao nasi tunaweka mchanga  ili kufidia kwani gunia la ufuta toka ni  kilo 140 lakini nikifika mjini kupima kwa kutumia mizani ya wenzetu hawa wenye mitaji mikubwa kuna kuwa na upungu wa kilogramu 10  hivyo kulazimika kuongeza ili kufikisha uzito unao takiwa kakini nasi tumeamua  kutumia mbinu hii ili kuepusha migogo” alisema  Mwakalonge.

 Naye Mkurugenzi wa kati kampuni ya General Traders ambayo imekuwa ikinunua zao hilo kutoka kwa wachuuzi Eden Katininda alikiri kuepo kwa kwa matatizo yoye mawili na kuchanganya mchanga na ufuta na kuhusu mizani alisema kuna baadhi ya wafanyabishara ama makampuni yanayo fanya uchakachuaji kwa lengo la kuwaibia wakulima.

Hata hivyo aliupongeza pamoja na kuwepo kwa tatizo hilo isinge kuwa vema kwa wachjuui na wakulima kuchanganya mchanga na uwele kwani bei ya zaao hilo linashuka dhamani kutokana na uchafu unao kuepo katika ufuta.

 Alisema kuwa licha ya gunia lenye uzito wa kilo 140 kuuzwa kwa shilingi 230,000/ lakini linauzwa kwa bei hiyo kutokana ubora wake kuwa chini, na kwamba Mkoa wa Mbeya una bahati kwani zao limekuwa likikomaa mapema tofauti na Mikoa mingine hivyo ni vema wakulima hao wakaitumia fursa hiyo kuwa na bidhaa yaenye kiwango kuliko kuafanya ujanja ambaop mwisho wake ni kuharibu.

No comments:

Post a Comment

Pages