FAINALI za
mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya Mikoa zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia
nchini(TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager zijulikanazo kwa “ Safari National
Pool Competition 2014” zinatarajiwa kuendelea tena wikii hii baada ya kusimama
kupisha mfungo wa Ramadhani.
Akizungumza
na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga
alisema mikoa inayotarajiwa kuendelea wiki hii ni pamoja na Mkoa wa kimichezo
wa Kinondoni,Tanga na Manyala ambayo itakamilisha fainali zake mwishoni mwa
wiki hii na kupata vilabu vitakavyowakilisha mikoa hiyo katika fainali za
kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Mikoa ambayo
imeshamaliza fainali za mikoa ni Lindi,Mwanza,Shinyanga na Pwani. Lindi klabu
bingwa atakayewakilisha mkoa huo katika fainali za kitaifa ni Blue Leaf Pool
Klabu na upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume ni Hassan Salumu na upande wa
kinadada ni Mwajuma Othman, Mwanza ni Klabu ya Billiard Pool Klabu na upande wa
mchezaji mmoja mmoja Wanaume ni Lamerk Omary (Ndala Ndefu) na upande wa Wanawake
ni Rukia Issa, Mkoa wa Shinyanga mabingwa ni New Stand Pool Klabu, upande wa
wachezaji mmoja moja Wanaume ni Paul Filaki na upande wa Wanawake ni Sada
Tullah, Mkoa wa Pwani mabingwa ni Yakwetu Pool Klabu, upande wa mchezaji mmoja
mmoja wanaume ni Anold Djoef na upande wa Wanawake ni Fatma Kihongo.
Fainali za
kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika
Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni
Tabora, Shinyanga, Dodoma Mbeya, Iringa, Morogoro, Mwanza, Kagera, Manyara, Arusha,Tanga, Pwani, Ilala, Lindi, Temeke, Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment