Washiriki wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2014 wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yanayofanyika kwenye Hotel ya Picolo jijini Dar es Salaam, Jumla ya warembo 20 wapo mazoezini kujiandaa na shindano litakalofanyika ijumaa 15/08/2014 katika Fukwe za Escape One kwa kiingilio cha 10,000 na 30,000 kwa VIP.
Redd's miss Kinondoni 2014 wakiwa katika pozi.
Redd's miss Kinondoni 2014 wakionyesha pozi tofauti.
Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumsaka Redd’s Miss
Kinondoni, sasa limefikia patamu baada ya mambo yote kukamilika na
kinachosubiriwa ni siku tu ya mchuano wenyewe.
Akithibitisha hilo, Mratibu wa Redd’s
Miss Kinondoni, Husna Maulid, alisema kila kitu kimekamilika, huku warembo 20
watakaochuana wakiwa katika mazoezi makali.
Husna alisema, shindano hilo litakuwa la
kipekee kutokana na mengine yote yaliyowahi kufanyika na ana uhakika mkubwa
hata taji la Redd’s Miss Tanzania litatwaliwa na mrembo kutoka Kinondoni.
“Kwa sasa kinachosubiriwa ni siku tu na
warembo 20 wapo katika mazoezi makali kwa ajili ya shindano hilo.”
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika
katika Ukumbi wa Escape one uliopo Mikocheni, Dar es Salaam huku kukiwa na
burudani kali toka Malaika Band inayoongozwa na Christian Bella na mwanamuziki
wa kizazi kipya anaechipukia kwa kasi Young Suma.
Taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa
linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss
Tanzania, Brigitte Alfred.
Warembo wanaoshiriki shindano hilo
wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani,Ubungo na Dar Indian Ocean, huku
kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti
maalumu na pia watu mia moja watakaoingia wa kwanza watapata bia moja ya Redd’s
original bure kabisa.
Alisema tiketi kwa ajili ya shindano hilo
zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi jumatano ya juma lijalo sambamba na zawadi
mbalimbali toka kwa wadhamini wa shindano hilo
Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s
Original, Kitwe General Traders, CXC Africa,Picolo Hotel, Jambo Leo, Clouds FM,
Michuzi Media Group, Father Kidevu blog, Glitters Salon, EFM Redio na Habari
Mseto Blog.
No comments:
Post a Comment