Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Serikali imetenga fedha
zitagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri nasaha na kurekebisha watoto
walio chini ya umri wa miaka 18 vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa jamii nchini.
Kauli hiyo imetolewa na
Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Majira
toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa cha habari
“Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=”.
“Ni kweli tatizo hilo
lipo ndio maana Serikali imetenga fedha tayari ambazo zitagawiwa kwenye vituo
vyote nchi nzima” alisema Mwamwaja.
Mwamwaja alisisitiza kuwa
deni hilo litalipwa kweye mahabusi hiyo iliyoko Tanga.
Mahabusi hiyo ni miongoni
mwa vituo kadhaa vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii ndani ya Wizara ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Matumizi ya fedha hizo
ni pamoja na kushughulikia tatizo la maji na uhaba wa chakula kituoni hapo ili
kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto hao na kufikia lengo la kuwarekebisha
tabia zao ili wawe raia wema nchini.
Aidha, Mwamwaja
aliongeza kuwa fedha zilizotengwa si za
Mkoa wa Tanga tu bali ni kwa ajili ya vituo vya nchi nzima zikiwemo makambi ya
wazee wasiojiweza, mahabusi za watoto na kambi za kutibu wagonjwa wa ukoma.
No comments:
Post a Comment