NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’
amesema hatafunga ndoa mwaka huu kama alivyotangaza awali kutokana na kuuguliwa
na mama yake mzazi.
Awali Tunda alisema, anampango wa kufunga ndoa Octoba mwaka huu
bila kuweka wazi ni nani ambaye anatarajia kumuoa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Tunda Man alisema, kutokana
na kuuguliwa na mama yake ameamua kuhairisha ndoa hiyo mpaka mwakani hali ya
mama yake itakapoimarika.
“Mpango wa kuoa upo pale pale lakini kutokana na kuuguliwa na mama
kwa muda mrefu nimeamua kusogeza mbele mpaka mwakani na sio Octoba kama
nilivyokuwa nimepanga,” alisema.
Aidha, nyota huyo alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji
wa kibao chake kipya kinachojulikana kwa jina la ‘Hasara Roho’ ambayo
ameitengeneza kwa mtayarishaji mahiri, Manecky,” alisema.
Nyota huyo kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Msambinungwa’
alichofanya na mkali wa muziki huo, Ali Kiba licha ya kuwa na kazi nyingi
ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri.




No comments:
Post a Comment