Baadhi ya wajawazito wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba wa vitanda.
NA SYLVESTER DAVID
TAASISI
isiyo
ya kiserikali ya Society Watch,imeishauri serikali kupunguza gharama
za uendeshaji wa Ofisi za wizara badala yake zitumike kuwasaidia
wajawazito masikini nchini..
Hayo
yalisemwa jana na Mtendaji Mkuu wa taasisi
hiyo, Simon Nkondya katika mahojiano maalumu jijini Dar es salaam.
Nkondya
ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za akina mama wajawazito alisema
wameamua kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa
afya, serikali na viongozi wa taasisi binafsi kutokana na kuguswa na hali hiyo
na kuendelea kutafuta jitihada za kuinusuru unyanyasaji wa wanawake na
miundombinu za kuwafikisha katika
hospitali mbalimbali.
“Kama
viongozi wetu wakitumia magari ya serikali yenye gharama ya shilingi million 15
yatafanya pesa zingine kutumika katika huduma mbalimbali za kijamii ikiwezekana
kuboresha huduma kwa wajawazito tofauti na tafiti zinavyoonyesha kuwa wanatumia
gari za shilingi million 300”,alisema
Aliongeza
kuwa, Taasisi ya Society Watch linatarajia kuandaa tamasha la wajawazito nchini
ifikapo Desemba 14 mwaka huu ,Kuongeza juu ya ujauzito, kupunguza
vifo kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, kupunguza mimba za utotoni,
kukuza uzalendo na kuhamasisha wajawazito kupenda kujifungulia kwenye vituo vya
Afya-serikali.
Pia aliongeza kuwa taasisi imefanya tukio la
kuhesabu mashimo ya barabara kutokea Tabata Kimanga mpaka Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kwa kutumia fimbo ya Society Watch yenye ujumbe mbalimbali za
harakati za haki za binadamu lengo ni kujua adha na mitikisiko inayoweza
kuharibu ujauzito waipatayo wawapo barabarani na kugundua kuna idadi ya mashimo
27,253 , ambayo ni hatari kwa afya za
wajawazito.
No comments:
Post a Comment