Na
Rose Masaka, MAELEZO, Dar
es Salaam
SHIRIKA la Under The Same Sun
kwa kushirikiana na chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (TAS), kimeiomba Serikali kuangali au uwezekano wa kushirikiana na Jumuiya za Kimataifa ili kuunda kikosi kazi kitachosaidia shughuli za upelelezi ili kubaini chanzo cha mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
AidhaTaasisi hizo pia zimeitaka Serikali kuchukua hatua zinazostahili za kukomesha kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji na ukataji wa viungo vya mwili kwa watu wa jamii hizo ili waweze kuishi kwa amani kwani ni haki yao ya msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Bi. Ziada Nsembo amesema TAS imesikitishwa na vitendo hivyo vya kikatili kwa kuwa mauaji ya watu hao vinavyochochewa na imani za kishirikina miongoni wa mwa jamii.
Bi. Ziada alisema kuishi ni haki ya kimsingi iliyoanishwa katika Katiba yaNchi,
hivyo wanashangaa baadhi ya wana jamii wanachukulia Albino
kama ni watu wa sista hili kuishi na viungo vyao ni moja ya njia ya kujipatia utajiri,
imania mbayo ni potofu.
“Tumekuwa na msiba kutokana na kilio cha muda mrefu tunachotendewa, baadhi ya wenzetu wamepoteza viungo vyao vya mwili ikiwemo mikono pamoja na viungo vya sehemu za siri kutokana na imani za kishirikina zilizojengeka katika jamii”
alisema Bi Nsembo.
Kwaupande wake, AfisaHabariwa TAS Bw. Joseph
Torner amesema kuwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto wa miaka 15 Upendo Sengerema
wiki iliyopita cha kukatwa mkono wake wakulia chini ya kiwiko na watu watatu kijiji cha
Usinge mkoani Taborani cha kinyama na kusikitisha.
Torneraliongezakuwahilinitukio la pili kutokea ndani ya miezi mitatu na waganga wa kienyeji wamekuwa wakihusika katika matukio haya,
ambayo katika kipindi cha
karibuni matukio ya aina hii ya lisimama kutokana na wahusika kuogopa vyombo vyadola.
Torner alisema kuwa Serikali haina budi kufuta vibali kwa waganga wa kienyeji ili watu wenye ulemavu wangozi waweze kuishi bila hofu,
kwa ni wengi wao tayari wameathirika kisaikolojia na linarudisha nyuma maendeleo kwani watoto wanaogopa kwenda shule na watu wazima wanashindwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo.
Chama cha albino TAS na UTSS na wadau wengine wataasisi zisizo za kiserikali wanakusudia kufanya maandamano ya amani nchi nzima katika muda utaopangwa ili kuijulisha serikali iweze kuwasaidia kikamilifu.
No comments:
Post a Comment