HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2014

Wadau soka Sumbwanga waipa tano Mbeya City

NA KENNETH NGELESI,SUMBAWANGA

WADAU wa soka Mjini Sumbwanga wamefurahishwa uamuzi uliofanywa na timu ya Mbeya Cit FC wa kuipeleka timu hiyo na kufungua matawi katika ukanda wa Mikoa ya Rukwa na Katavi.

Katibu wa timu ya Mbeya City, Immanuel Kimbe amesema kuwa hatua hiyo ni ya kupongezwa na kwamba inapaswa kuigwa na vilabu vingine.

Walisema kuwa kitendo hicho cha Mbeya City kukanyaga katika ardhi ya Mikoa ya Rukwa na Katavi kimewafuta kiu ya kuiona timu ya ligi kuu ambapo kwa zaidi ya Miaka 20 iliyopita wakazi wa mji wa Sumbawanga hawajawai kuona timu ya ligi kuu ikifika mjini hapo tangu enzi za Ujenzi Rukwa.

Miongoni  mwa wadau hao ni Ntori Mwambusi ambaye ni Mwenyekiti Mbeya City tawi la Sumbawanga mjini, alisema kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa  timu hiyo kufika katika Mikoa hiyo inaonyesha ni jinsi gani wamedhamiwa.

Alisema kuwa mashabiki wa soka katika mjiji wa Sumbwanga wamekuwa wapenzi wa timu hiyo tangu ilipoanza ajapo wengi wao wao walikosa fursa ya kuweza kuiona moja kwa moja hivyo kitenda cha kufika kitawongezea morai ya kuipenda na kuendelea huku wakiwashawishi watu wengini kuishabikia timu hiyo kwani imeonysha kuwa jali kwani kitendo hicho kitaifdanya timu hiyo kuendelea kupata mashabiki lukuki.

‘Una jua Sumbawa wana tuna penda sana soka, lakini sasa tuna muda wa miaka 20 imepita hatuja kushuhudia mchezo wowote wa ligi na walau kutembelea na timu yoyote inashiriki ligi kuu n indo mara ya kwanza’ alisema Ntori.

Yahani hata vilabu vikubwa ambavyo vinajiita vinam asahabiki nchi nzima havijawai kuja kutembelea mashabiki wake hivyo kitendo cha Mbeya City kufika kimetupa morali wa kuendelea kuipenda zaidi na tuna kila sababu ya kujnivunia” alisema Ntori

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kufika kwa timu hiyo katika mji wa Sumbwanga iwe chachu ya uongozi wa soka katika Mkoa wa Rukwa na kwamba ni fursa pekee ya kujua njia walizo pitia Mbeya City mpaka kufika hapo walipo fikia.

Mdau mwingine ambaye alionyesha  kuguswa na ujio wa kikosi cha timu hiyo mjini hapa ni Godfrey Kalemya katibu wa timu ya Mazwi FC inayo shikiriki ligi daraja la nne Mjini hapa ambaye alisema kuwa mara ya mwisho kuona timu ya ligi kuu ni mwaka 1994.

Alisema kuwa ujio wa timu hiyo ni faraja kwao kwani inonyesha ni jinsi gani uongozi wa Mbeya City umetambua mchango wa mashabiki katika Mji wa Sumbawanga.

Hata hivyo alitaka uongozi Mbeya City kuendelea kuisimamia vyema timu hiyo  kama msimu uliopita ili iweza kushika nafasi ya kwanza ama ya pili ili iweze kushiriki michunoano ya kimataifa, na kwamba zoezi la kutembea mashabiki lifanywe kwa mikoa ya yote ya Tanzania ili kuendelea kuzoa mashabiki.

Naye katibu wa Mbeya City Kimbe alipongeza mapokeza mazuri waliyo ya pata kutoka kwa mashabiki wa timu yake na kwamba wapo tayari kuileta leta timu hiyo kwa mara nyingine pindi watakapo pata nafasi.

Kimbe alisema kuwa haikuwa kazi raisi kufikia mafanikio hao lakini kwa uongozi dhabiki pamoja na ushabiki wa dhati kutoka kwa wadau mbalimbali  wakiwemo wa Sumbanga ndiyo sababu timu hiyo kufika hapo ilipo.

Mara baada ya kufungua tawi hilo la Sumbwanga lenye kauli mbiu “Umoja ni Chachu ya Mafanikio” ulifanyika mchezo wa kirafiki kati ya Mbeya City na timu ya Wajasiriamali ya Mazwi FC ya mjini Sumbawanmga ulio pigwa katika dimba la Nelson Mandela ambao ulimazika kwa Mbeya City kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

 Katika mchezo huo ambao ulishihudiwa na maelfu ya mashabiki kutoka mjini Sumbawanga magoli ya Mbeya yalifungwa na Erick Mawala,Abdalah Self kipindi cha kwanza na goli la tatu liliwekwa kimyani na Temy Felix kipindi cha pili cha mchezo ambapo kocha Juma Mwambusi akishirikiana na kocha msaidizi Jabir waliwachezesha wachezaji wote.

Mara baada ya mchezo huo kikosi cha Mbeya City,benchi la Ufundi na bodi ya timu hiyo ikiongozwa na mwenyekiti Musa Mapunda pamoja na Madiwani 4  kilitarajiwa kusafari hadi mji Mpanda ambapo jana kwa ajili ya mcheza wa kirafiki na Mpanda United,ambapo safari hiyo ikiwa na lengo la kufungua matawi,kusaka mashabiki.

No comments:

Post a Comment

Pages