HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2014

AZMA, "MVUA YA MAPENZI' NIMEFANYA NA NAKAAYA

NA SYLVESTER DAVID 

MASANII maarufu wa muziki wa Hip Hop nchini, Azma M ponda ‘Azma’, amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa ujio wa wimbo mpya aliomshirikisha Nakaaya Sumari ‘Nakaaya’ uitwao ‘Mvua ya upendo’ ambao utawajia hivi karibuni.

Akizungumza  na Tanzania daima jana jijini Dar es salaam,alisema,wimbo huo ambao ni waina yake umebeba hisia za mapenzi ya kweli.

Azma ambaye yupo katika kundi la muziki la ‘Tamaduni’ lenye makazi yake jijini Dar es salaam aliwahi kutamba na nyimbo kama, Bongo Fleva inakufa,We never give up na Utata wa Katiba,alisema wimbo huo umefanyika Jijina Arusha katika studio ya Noiz Makers.

“Wimbo wangu umebeba radha na ujumbe muhimu katika maisha ya halisi ya mahusiano,mashabiki wangu waupoke naamini wataupenda sana,”alisema.

 Pia alisema juzi alikuwa katika ziara ya kuzunguka mikoa 12 nchini kwa ajili ya mauzo ya albamu ya wimbo wake wa‘Love Stories’ kutokana na mfumo duni usambazaji nchini na kufanya utafiti wa soko lake la muziki.

No comments:

Post a Comment

Pages