Baadhi ya warembo wanaoshiriki Shindano la Redd's Miss Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja.
NA MIKA
NDABA
SHINDANO la Redds Miss Kinondoni linatarajia kuwashusha jukwaani warembo 20 watakaowania taji hilo litakalo fanyika Agosti 15, mwaka huu katika Ukumbi wa Escape 1, Mikocheni Dar es Salaam.
SHINDANO la Redds Miss Kinondoni linatarajia kuwashusha jukwaani warembo 20 watakaowania taji hilo litakalo fanyika Agosti 15, mwaka huu katika Ukumbi wa Escape 1, Mikocheni Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Shindano hilo, Innocent Melleck,
alisema warembo hao tayari wameiva na kinachosubiriwa ni kesho tu kujua mshindi
ni nani kati yao.
“Kinachosubiriwa
ni siku tu kwani warembo hao wataondoka na zawadi za kila aina na za kuvutia, pia
kuna burudani mbalimbali ikiwemo Malaika Band wakiongozwa na Christian Bella
pamoja na msanii wa kizazi kipya Young Suma watapagawisha mashabiki” alisema.
Melleck
alisema, taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka,
ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.
Warembo
wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian
Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh
30,000 viti maalumu na watu mia moja wa kwanza kununua tiketi mlangoni kupata
Redd’s Original moja ya bure kabisa.
Aidha
alisema, warembo hao wametunga wimbo
mmoja maalum kwa ajili ya kuhamasisha uzalendo, amani na umoja wa Taifa la
Tanzania, tunawaomba wapenzi wa burudani na tasnia ya urembo nchini kuja kwa
wingi kushuhudia namna warembo wa Kanda ya Kinondoni walivyojiandaa kwa
shindano hili.
Kwa upande
wake mkuu wa itifaki wa kamati ya miss Tanzania Albert Makoye aliwaasa
washiriki hao kujiandaa kisaikolojia na kusema kanda ya Kinondoni kwa mwaka huu
inaonyesha kujiandaa vyema zaidi sanjari na kuwa na warembo ambao ni nadra sana
kuwaona popote pale nchini.
Nao warembo
wanaoshiriki shindano hilo, walikutana na waandishi wa habari kwa nyakati
tofauti, ambapo kila mmoja alijitamba ataondoka na taji hilo.
Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s Original, Zanzi, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo, Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu blog, Gletters Salon, E- FM, Habari Mseto Blog, Picolo Hotel na Uhuru Marathon Tanzania.
No comments:
Post a Comment