DAR ES SALAAM, Tanzania
WATU watatu wamefariki Dunia jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na kuchomwa moto na
wananchi kwa tuhuma za wizi wa piki piki.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 6:30 mchana
huko maeneo ya Zingiziwa kata ya Chanika.
Nzuki alisema watu watatu wanaume wasiofahamika wenye umri kati ya miaka 25 na 30 wameuawa baada ya kushambuliwa na wananchi
waliojichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga kwa fimbo na mawe hadi kufa kisha
kuwachoma moto kwa tuhuma za kumpora Zablon Kerekaro (18) mkazi wa Rubakaya
aliyekuwa akiendesha piki piki yenye
namba za usajili T – 376 CWX aina ya
Fekon yenye rangi nyekundu.
Alisema Kerekaro majira ya saa sita mchana alitoka
Chanika ili ampeleke Videte maeneo ya
Zingiziwa, wakiwa njiani abiria huyo alimuomba asimame ili ajisaidie
baada ya kusimama ghafla abiria huyo alimkaba.
Kwa mujibu wa Nzuki
baada ya tukio hilo, walitokea watu wengine wawili na kumdhibiti kumfunga kamba mikononi na miguuni kisha kumlaza kichakani huku wakimpiga ngumi na mateke,
hatimaye waliondoka na pikipiki hiyo.
Kwa mujibu wa Nzuki, wakati tukio hilo,linaendelea dereva mmoja wa
bodaboda ambaye bado hajafahamika alikuwa akilishuhudia tukio hilo, ndipo
alianza kuwafuatilia wezi hao huku akifanya mawasiliano na madereva wenzake hatimaye kundi kubwa la waendesha pikipiki
likaanza kuwafuatilia na kuwakuta wamejificha kwenye kichaka wakiwa na pikipiki
walizopora.
Nzuki alisema waendesha bobaboda hao walianza
kuwapiga hadi kuwauwa na kuwachoma moto
sehemu kubwa za miili yao hali iliyosababisha
kushindwa kutambuliwa miili yao.
Nzuki alibainisha kuwa sehemu ya tukio zilikutwa
hirizi tatu nyekundu zilizozungushiwa shanga zinazosadikiwa kupatikana kwa wezi
hao kabla hawajauwawa.Miili ya maiti hizo zimehifadhiwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
No comments:
Post a Comment