Mwenyekiti
wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya Sultan Thawer (kushoto), akitoa taarifa
kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa
wa Mbeya juzi katika Ukumbi Mkapa jijini Mbeya. (Picha na Kenneth Ngelesi)
NA
KENNETH NGELESI, MBEYA
HOSPITALI
ya Aga Khan ya Mbeya imetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali na vituo vya
afya katika Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya vyenye thamani ya zaidi ya
shilingi Milioni 300.
Msaada
huo ulikabidhiwa juzi na uongozi wa Hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro kwa niaba ya Halmashauri husika katika hafla iliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini hapa.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo mratibu wa Mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja(JHI)
Mkoa wa Mbeya, Abel Kide, alitaja Halmashauri zilizonufaika na mradi huo kuwa
ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Kyela,
Mbozi na Momba.
Kide
ambaye pia ni Meneja Hospital ya Aga
Khani Mkoa wa Mbeya alibanisha Hospitali na zahanati zinazopatiwa vifaa hivyo
kuwa ni Zahanati ya Ngana na Hospitali ya Wilaya ya Kyela(Kyela), Zahanati ya
Iyunga na kituo cha Afya Kiwanja Mpaka(Mbeya jiji), Hospitali ya Wilaya ya
Mbozi(Vwawa)na Zahanati ya Ivuna iliyopo wilayani Momba.
Katika
hatua nyingine Meneja huo ilivitaja vifaa hivyo kuwa ni Vitanda vya
kujifungulia wajawazito, vitanda vya wagonjwa wa kawaida, Mashine za kuchemshia
vifaa vya hospitalini, Mashine ya kumpa joto mtoto aliyetoka kuzaliwa, Mashine
ya Ultra Sound,Mashine ya kumtolea uchafu mtoto mchanga,mashine za kupima
uzito, joto, urefu na shinikizo na kwamba vyote jumla vinagharimu zaidi ya
shilingi Milioni 300.
Kide
alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuboresha afya ya mama mjamzito, mtoto
mchanga na mtoto aliyechini ya miaka mitano ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma
za afya karibu na wananchi hususani kuokoa vifo vinavyotokea wakati wa
kujifungua.
Akipokea
vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alipongeza Hospitali ya Aga
Khani kwa Msaada waliotoa katika Halmashauri hizo na kuziomba taasisi zingine
kuungana na Serikali katika mpango wa kuhakikisha vifo vya Wanawake wajawazito,
watoto wachanga na waliochini ya umri wa miaka mitano vinapungua.
Kandoro
alisema mkakati wa kupunguza vifo hivyo hautafanikiwa ikiwa utakuwa ukifanywa
na sekta moja ya afya pekee bali kwa kushirikisha sekta zingine binafsi
za serikali, viongozi wa dini na vyombo vya habari.
Aliongeza
kuwa ili kukomesha kabisa vifo hivyo, Halmashauri zitenge bajeti za kununua
mfumo wa huduma tembezi(Mobile clinic) ili ziweze kufika hata maeneo ambayo
hakuna huduma ya afya kwa kuwasogezea wananchi huduma ili waweze kupata msaada
wa matibabu wakati wowote.
Sambamba
na kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alizindua Mpango wa utekelezaji wa
kupunguza kasi ya vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi, watoto na watoto
waliochini ya umri wa miaka mitano.
Kandoro
aliongeza kuwa mkakati huo ni maagizo ya Rais wakati wa uzinduzi wa kitabu cha
Mkakati wa kitaifa uliofanyika Mei 15 Mwaka huu ambapo aliagiza Kila Mkuu wa
Mkoa kuutafakari mkakati huo kulingana na mazingira wanakotoka.


No comments:
Post a Comment