HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2014

BENKI YA CRDB NA TEKNOLOJIA KATIKA SOKA


Shabiki wa soka akinunua tiketi ya Kieletronic katika mashine maalum iliyofungwa katika tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam FC utakaochezwa Septemba 14 kwenye Uwnja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela  akinunua tiketi ya kieletroniki kutoka katika mashine maalum iliyofungwa katika tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kushuhudia mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam utakaofanyika Jumapili Septemba 14.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Benki ya CRDB, imeendelea kuimarisha ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika upatikanaji wa Tiketi za kieelectroniki kwa wapenzi wa soka.  

Mfumo wa kupatikana Tiketi kwa njia ya Kielectroniki unalengo la kuongeza mapato ya TFF na hata kwa Vilabu vinavyoshiriki katika ligi inayodhaminiwa na TFF.

Jumapili kesho, tarehe 14/9/2014, Mfumo wa kielektroniki utatumika tena kuwauzia  wapenzi wa soka tiketi kwa ajili ya kwenda kushuhudia mechi kali kati ya Yanga na AZAM, kuwania Ngao ya Hisani.Mtanange utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela amesema kuwa katika kuwapunguzia wapenzi wa soka usumbufu wa kupata tiketi wanapotaka kwenda kuangalia mechi mbalimbali za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Benki ya CRDB, inawawezesha wapenzi wa soka kununua tiketi kupitia Simu zao za Mkononi yaani kwa Simu Banking, ambapo mteja/ mpenzi wa soka aliyejiunga kwenye huduma ya Simbanking atabonyeza *150*03# na kisha atakamilisha process zingine na mwisho atapata namba ya tiketi yake  atakayo weza kuiprint kwenye Mashine Maalum zilizofungwa kwenye vituo 29 hapa jijini Dar es Salaam, ikiwemo kwenye ATM za matawi ya Benki ya CRDB Azikiwe, Holland, Vijana, Kariaakoo, Mbezi Luis Agency, Tegeta, Quality Center, Mbagala na Pugu.

Pia Mpenzi wa Soka anaweza Kuprint Tiketi yake ya Kieletroniki (e-ticket) kupitia mashine maalum zilizofungwa  kwenye Offsite ATM za Benki ya CRDB kwenye maeneo yafuatayo: Kobil SabaSaba-Barabara ya Kilwa, Hospitali ya Temeke, Camel Station Tabata Junction  na Kawe.

Aidha mashabiki wa Soka wanaweza kununua tiketi ya kielektroniki kupitia huduma ya M-Pesa iliyo unganishwa na mfumo wa ATM za Benki ya CRDB. Mpenzi wa Soka anayetaka kununua Tiketi atabonyeza *150*03*02# kwenye simu yake kisha  kuendelea na hatua zinazofuata kukamilisha muamala ambapo hatimaye atapata namba ya tiketi na kwenda Kuprint kwenye Mashine Maalum zilizotajwa hapo juu.

Kwa upande mwingine, Maofisa  wa TFF, walisema kuwa batch elektroniki tiketi zaweza PIA kupatika katika vituo vinavyo simamiwa na TFF katika  Uwanja wa Karume, Mgahawa wa Steers-Mtaa wa Ohio, Dar live-Mbagala, Buguruni sheli, Oilcom Ubungo, Sokoni Kariakoo, Breakpoint Kijitonyama/Makumbusho stand, Banana Ukonga, Namangan a Mwenge

Mwandishi wa habari hizi ameshudia wapenzi lukuki wa soka wakinunua/wakiprint tiketi za kieletroniki kwenye mashine iliyofungwa kwenye tawi la Benki ya CRDB Azikiwe.

No comments:

Post a Comment

Pages